ESTER AKUTWA NA SHATI LA DUDE

Msanii anayekuja juu kwa kasi kwenye gemu la filamu Bongo, Ester Kihama amenaswa akiwa ametinga shati linalodaiwa kuwa la staa wa kiume wa filamu, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
 
Msanii anayekuja juu kwa kasi kwenye gemu la filamu Bongo, Ester Kihama.
Mpashaji wetu alisema alimnasa mwanadada huyo akiwa anakatiza mitaani na shati hilo ambalo mara nyingi analivaa Dude akamfotoa picha za kutosha kwani kitendo hicho kilizua maswali kwa watu kwamba inakuwaje msanii huyo avae shati la mume wa mtu mwenye familia yake?
Alipoulizwa Ester kuhusiana na habari na picha hizo alijitetea hivi; “Jamani  hilo shati nililivaa wakati nikiwa narekodi filamu na hata ikitoka mtaona kwa vile tuliigiza kama mke na mume lakini hakuna kitu kingine chochote.”

Post a Comment

Previous Post Next Post