RAY: KANUMBA ALIKUFA NA NYOTA YANGU!

Msanii Vincent Kigosi ‘Ray’ amekiri kwamba kufariki kwa Steven Kanumba kumemsababishia kuporomoka kisanaa na kiuchumi kwa kukosa ushindani thabiti kwenye game.
 
Msanii Vincent Kigosi ‘Ray’.
Akizungumza na mwandishi wetu katika mahojiano maalum hivi karibuni, Ray alisema Kanumba alipokuwa hai, alikuwa na changamoto kubwa katika ubunifu wa kazi na hata ushindani wa maisha ya kawaida.
Akatolea mfano baadhi ya mambo yaliyokuwa yaking’arisha nyota yake kuwa ni pamoja na kushindana katika kumiliki vitu kama magari, silaha binafsi (bastola) na filamu zenye ubora, kitu ambacho kwa sasa haumizi kichwa baada ya kuondoka kwa Kanumba.
 
Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
“Kila kitu kinapokosa ushindani maana yake kinapoa, kuondoka kwa Kanumba limekuwa pigo kubwa sana kwangu kwani sina tena mtu wa kunipa changamoto kama kipindi kile, ni kama nyota yangu imefifia,” alihitimisha Ray.

Post a Comment

Previous Post Next Post