Akiongea katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds Fm Alhamisi 
hii, Daktari wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Muheza mkoani 
Tanga, Dk. Abas Mussa, amesema jana majira ya mchana walimpokea mgonjwa 
huyo akiwa hana sehemu zake zote za siri.
“Jana tulimpokea mgonjwa katika chumba kidogo cha upasuaji akiwa 
ameletwa kwa ajili ya kushonwa,” alisema Dk Abas.  Mgonjwa huyo baada ya
 kumkagua tuligundua kwamba ameondoa sehemu zake za siri, alijieleza 
kwamba yeye mwenyewe ana tatizo la akili na amehisi kwamba amejiwa na 
vitu kama mashetani au majini ambayo yalimuamuru kuondoa sehemu zake za 
siri. Tuliona huyu mtu alitumia kitu chenye ncha kali, mfano wa kisu 
ambacho aliweza kujiondoa uume wake pamoja na korodani mbili,”
Aliongeza, “Mteja wetu huyu alikuja katika hali ya kumwagika damu, 
kutokana na jeraha hili kubwa tukaamua kumpeleka katika chumba cha 
upasuaji, kwa ajili ya kufanyiwa matibabu zaidi, sehemu za siri 
hazikuwepo kabisa, kwa maana hata ushahidi wa kuziona zikiwa zimebebwa 
pembini haupo, kwa hiyo itakuwa baada ya kuziondoa zilisalia huko huko 
ambako aliziondoa, ilibakia sehemu ya wazi ambayo iliweza kushonwa na 
kurudi kawaida, tulicho jitahidi ni kuhakikisha kwamba hatoki tena damu,
 lakini pia tumeshona yale majeraha ili aweze kupata uwazi wake wakutoa 
mkojo, na pia kwa sasa anaendelea vizuri,”
Post a Comment