Benki ya Dunia hatimaye yampata Rais mpya, lakini
Baada ya upinzani wa wazi wazi kutoka kwenye nchi zinazoendelea kiuchumi, hatimaye Benki ya Dunia (WB) imempata Rais mpya aliyetarajiwa na wengi, Dkt. Jim Yong Kim, raia wa Marekani mwenye asili ya Korea Kusini.
Uchaguzi huo umelalamikiwa na baadhi ya viongozi wa nchi zinazoendelea ambao wamesema hufanyika kwa usiri mkubwa na kwa utaratibu unaokanganya kwa lengo la makusudi la kuufanya potofu, wenye upendeleo na usio wa wazi.
Pamoja na Rais Obama kukiri madai ya nchi nyingi ya kwamba ni wakati muafaka kwa mabadiliko kufanywa katika kiti hicho, wachambuzi wa mambo wanajua fika kuwa siasa za ndani za Marekani zimeathiri maamuzi na Rais Obama ilimlazimu kumpigia chapuo Raia wa Marekani kushikilia kiti hicho ili kuziba mwanya wa sababu ya kupingwa kwenye kampeni na wapinzani wake wa kiti cha Urasi wa Marekani unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba, 2012.
Rais wa sasa, Robert Zoellick ndiye rais wa Benki hiyo kwa sasa na Dkt. Kim ataanza rasmi uongozi wa kiti hicho cha Urais ifikapo Julai Mosi, mwaka huu kwa kipindi cha miaka mitano.
Lakini walilokuwa wanajiuliza baadhi ya watu ni kama Dkt. Kim ambaye fani yake ni Udaktari wa Binadamu na ameongoza mashirika na kushiriki kuanzisha shirika lililojishughulisha na maendeleo ya kijamii kwa nchi zinazoendelea.
Ili kujaribu kupata majibu, John Ydstie shirika la habari NPR anasema anasema, "the top job at the World Bank has usually been reserved for financiers, economists or political heavyweights. There have been questions about whether Dr. Kim has the mindset to 'allocate scarce resources' as a banker or economist might do, or whether he's got the political skill to get things done at a global institution that has 187 member nations. But others have praised his qualifications, saying that Dr. Kim's experience makes him ideally suited for the job and that it is time for a development professional to lead the world's largest development agency."
Kuhusu kushindwa kwa azma ya nchi zinazoendelea kiuchumi kumweka mtu kutoka eneo lao, Ydstie anasema, "in the end the U.S. candidate prevailed because the U.S. has the greatest number of votes at the bank and it also has the support of Europe, which has the second largest bloc of votes."
Tutasubiri kuona hatua zitakazochukuliwa na muungano wa kiuchumi wa nchi zinazoendelea, BRICS na azma yao ya kuanzisha benki yao.
Post a Comment