JACQUELINE WOLPER ABADILI DINI





Msanii Maarufu wa filamu Tanzania, Jacqueline Wolper amebadili dini na kuwa Muislam baada ya kuchumbiwa na kununuliwa gari la kifahari na mwanaume anayeitwa Dulla au "Dallas"
“Ni kweli nimebadili dini wiki mbili zilizopita baada kumpata mchumba ambaye tunatarajia kufunga ndoa hivi karibuni,” alisema Wolper.
Aidha, msanii huyo amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kumchunguza kwa muda mrefu mchumba wake huyo na kugundua kuwa ana nia nzuri kwa upande wake hivyo kukubali kumfuata katika dini yake.
Pia, Wolper amesema kuwa yeye na mchumba wake huyo wameshaanza kufanya taratibu za kupata baraka za wazazi wa pande zote mbili ili kuweza kufanikisha azma yao ya kufunga ndoa.
“Dallas ameshafika kwa wazazi wangu na hata mimi nimeshaenda kutambulishwa kwao, kilichobaki ni kufunga ndoa tu,” alisema Wolper kwa kujiamini.
Baada ya Wolper kubadili dini na kukubaliana na mchumba wake kufunga ndoa, mwanaume huyo alijikunja na kumnunulia msanii huyo gari la kifahari aina ya BMW X6 ambalo anatanua nalo mitaani hivi sasa.
Gari la kifahali analotembelea mwanadada huyu kwa sasa.
Habari kwa hisani ya PEKUA TZ

2 Comments

  1. mnh hana lolote huyooo, wolper the way anavojiachia na mavazi ya kimalaya, leo abadili dini awe muislamu kabsaaaa? Ataweza?
    Hata ivo uislamu haumkubali mtu kuingia kwa kumfuata mtu tuu bali uingie kwa matakwa ya nafsi sio kisa eti kapata mchumba muislamu ndio amfate .
    Allahu yaalam mungu ndie ajuaye nia yake, kila ajae kwa shari aijua yake nia.
    kama hayuko siriaz mungu atampatiliza.
    tunakukaribisha dini yenye mwongozo wote wa maisha.
    Takbiiiiiiiiiiiiirrrrrrrrrr
    Allahu akbar.

    ReplyDelete
  2. ni kweli usemayo dini ya kiislam haifatwi kwasababu ya mapenzi ya kumpenda mtu, bali dini ya kiislam inafatwa kwa imani ya kweli, kusoma na kuyakinisha kwa kumjua mungu wa pekee mmoja asie mshirika. ila hukuwa sahihi kuanza kumsema kwama amezowea kuvaa vivazi vya kimalaya, haifaii kutumia lugha hii...kumbuka Mungu anasamehe yote yaliyopita kabla ya yeye hajaingia katika uislam. na ni Mungu pekee ndie anaejua nafsini mwake. tunakupokea dada yetu kwa mikono miwili, inshaallah if u have anything to ask kuhusu dini yetu, au matatizo yoyote tunakukaribisha..hakika waislam ni ndugu, nawe ni ndugu yetu...sialone@yahoo.com

    ReplyDelete

Post a Comment

Previous Post Next Post