VIONGOZI WA DINI WAPIGWA MSASA KUHUSU SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani
Khijjah akizungumza na viongozi mbalimbali wa dini
kuelezea umuhimu na ushiriki wao katika kufanikisha sensa
ya watu na makazi itakayofanyika kitaifa mwezi Agosti
mwaka huu wakati wa mkutano wa viongozi wa dini
unaoendelea jijini Dar es salaam.
Baadhi ya viongozi wa dini wanaoendelea na mkutano wao
jijini Dar es salaam wakipitia vitabu na vipeperushi vyenye
jumbe mbalimbali kuhusu zoezi la sensa ya watu na makazi
litakalofanyika nchi nzima mwezi Agosti mwaka huu baada
ya wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoa semina
fupi kuhusu ushiriki wa viongozi hao katika kufanikisha
sensa hiyo .
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini
wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu mkuu wa Wizara ya
Fedha na uchumi Ramadhani Khijjah alipokuwa
akizungumzia umuhimu wa sensa ya watu na makazi 2012
na namna serikali ilivyojipanga kukamilisha zoezi hilo kwa
ufanisi.
Mkurugenzi mkuu ofisi ya taifa ya takwimu Dkt. Albina
Chuwa akisisitiza jambo kuhusu sensa ya watu na makazi
itakayofanyika mwaka huu wakati wa semina ya viongozi wa
dini jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani
Khijjah (kushoto) akiandika maswali yaliyoulizwa na viongozi
wa dini kuhusu namna serikali ilivyojipanga kukamilisha
sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti 2012.
Wengine ni mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu
Dkt. Albina Chuwa (katikati) na kamishna wa sensa Bi.
Hajjat Amina Mrisho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani
Khijjah (kushoto) akizungumza jambo na mkurugenzi mkuu
wa ofisi ya taifa ya takwimu Dkt. Albina Chuwa wakati wa
mkutano wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea jijini
Dar es salaam. Ofisi ya taifa ya takwimu imekutana na
viongozi hao kufuatia umuhimu na ushawishi wao katika
jamii ili waweze kushiriki kikamilifu katika kufanikisha sensa
ya makazi itakayofanyika mwezi Agosti 2012.
Post a Comment