WACHANGIA MFUKO WA KUSAIDIA WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO)


WACHANGIA MFUKO WA KUSAIDIA WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO)





watu wenye ulemavu wa ngozi wakiingia katika viwanja vya Mnazi Mmoja kumalizia maandamano yao yaliyoanzia katika viwanja vya Leaders jana, maandamano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Badef kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia albino nchini


Mbunge wa viti maalum Viti Maalum Mh.Shaimaar Kwegyr akisalimiana 


na washiriki wa maandamano hayo mara baada ya kufika katika 


viwanja vya Mnazi mmoja leo.
Shilingi milioni mbili zimekusanywa katika Harambee ya kusaidia kampeni ya
 kufanikisha maendeleo ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini iliyofanyika 

leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja.


Waliochangia fedha hizo ni Waziri wa Afya na Usatwi wa Jamii Mh.Dkt. Hadji 


Mponda aliyetoa milioni moja,Meya wa Manispaa Kinondoni Ndg.Yusuph 
Mwenda alitoa laki tano huku Mbunge wa Viti Maalum Mh.Shaimaar Kwegyr 
akitoa laki tano.
Akizungumza na watu waliojitokeza katika matembezi hayo Mwenyekiti wa 


Taasisi inajishughulisha na maendeleo ya watu wenye ulemavu iitwayo Badef, 


Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mh.Salum Barwany ambae Mbunge wa Lindi Mjini 


alisema kuwa shilingi milioni 500 zinahitajika.

Mh.Barwany alisema kuwa walemavu wa ngozi wanakabiliwa na tatizo la 


kansa ya ngozi ambayo inawashika kiurahisi zaidi kutokana na ngozi yao


 hivyo fedha hizo zitasaidia kuwanunulia mahitaji muhimu watu hao.
Alisema kuwa pia wanakabiliwa na tatizo la elimu kwa kuwa watu wenye 


ulemavu wa ngozi wana tatizo la kuona mbali hali inayowafanya kushindwa 


kuona vema darasani hivyo wanahitaji msaada maalum.
Alisema kuwa hizo ni moja kati ya changamoto ambazo jamii inatakiwa 


kuwasaidia walemavu hao kukabiliana nazo ambapo ili kufanikisha hilo kuna 


haja ya kufanya utafiti.
Alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kufanya utafiti wa kubaini namna ya 


kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi katika nyanja za elimu, kijamii na 


hata uchumi.
Pia Mh.Barwany alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kuwasafirisha kiurahisi 


albino ambao watakuwa na dalili za kansa ya ngozi ili kuwahi katika hospitali 


za rufaa kwa ajili ya matibabu.
“ Kwa sasa sisi walemavu wa ngozi tunahitaji milioni 500 ili angalu tuweze 


kusimamia na kujipatia mahitaji yetu muhimu ya kiafya hapa nchini, hivyo 


wanajamii tunaomba tusaidiane katika hilo tafadhali” alisema Barwany.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alitakiwa kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa 


Jamii Mh.Dkt.Hadji Mponda ambae hakuwepo na hivyo aliwakilishwa na 


Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda.
Maandamano yalianzia Viwanja vya Leaders na kumalizikia viwanja vya 


Mnazi Mmoja.
Vilevile unaweza kuchangia kupitia: Mpesa Namba; 0769696999, Airtel Money Namba; 0688858535, TigoPesaNamba; 0655029595 au kwenye akaunti ya BADEF (CRDB Bank, Lumumba Branch Akaunti Na. 0150278228900).
Habari kwa hisani ya:- http://dj-sek.blogspot.com

Post a Comment

Previous Post Next Post