Geofrey Nyang’oro
MKURUGENZI wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika amesema chama chake hakitawataja wabunge wa CCM wanaotarajia kuhamia Chadema.
Mnyika alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana akijibu kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Nape Nnauye, aliyekitaka chama hicho kiwataje wabunge wanaotaka kuhamia Chadema.
Nape alisema hayo baada ya Chadema kudai mawaziri na wabunge lukuki wa CCM wanatarajia kujiunga Chadema.
Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo alitaja msimamo wa chama hicho kutowataja mawaziri na wabunge 70 wanaotarajia kuihama CCM kwa madai ya kukwepa mbinu za CCM za kuwazuia.
Alisema katibu huyo wa Itikadi na uenezi wa CCM anajua mchakato wa vigogo waliotaka kuhamia Chadema wakati wa uchaguzi mkuu 2010 na mbinu zote zilitumika kuwazuia.
“Mimi ninajua sababu zilizofanya mpango wa vigogo kutoka CCM kujiunga na Chadema wakiwamo wabunge na mawaziri kukwama kwani wakati huo nilikuwa kaimu katibu mkuu na nilihuduria vikao vyote ndio sababu ninajua na pia ninajua kuwa naye anajua akitaka niseme nitasema,” alisema Mnyika.
Katika kikao cha jana Mnyika alibainisha kuwa chama hicho kinaendelea na mchakato wa operesheni za kujenga chama ambapo kwa sasa kinatarajia kufanya operesheni katika mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara.
Alisema hatua ya kupeleka chama hicho kusini imezingatia falsafa ya chama inayoamini katika nguvu ya umma ambapo lengo ni kuunganisha nguvu za wananchi kudai haki zao.
“Mabadiliko ya Mawaziri hayawezi kuleta tija katika nchi hii njia peke ni kukiondoa CCM madarakani na hili litaendelea kwa kupokea wananchama wapya kutoka CCM na wasio na vyama,” alisema Mnyika.
Alisema kwa sasa chama kinaendesha kampeni ya vua gamba vaa gwanda na kwamba dhana hiyo imeonyesha mafanikio kutokana na CCM kushindwa kuwawajibisha mawaziri walioshindwa kutimiza wajibu wao.

Chanzo:- Mwananchi.
Post a Comment