Zaidi ya shilingi bilioni 24 zinatarajiwa kukusanya katika Halmashauri
ya Wilaya ya Morogoro kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato kwa kipindi
cha mwaka wa fedha 2012/2013.
Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 1.23 ni kutoka mapato ya ndani ya
Halmashauri,\ ruzuku kutoka Serikali kuu ni shilingi bilioni 19.5
na
miradi ya maendeleo shilingi bilioni 4.8.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Eden Munisi na Mwenyekiti wa
Halmashauri Bi Kibena Kingo wamesema hayo wakati wakitoa mapendekezo ya
makadirio ya Bajeti ya mapato na matumizi ya kawaida, mishahara na
miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2012/2013 katika kikao Baraza la
Madiwani kilichofanyika wilayani humo.
Kiwango hicho cha Bajeti kimeongezeka kwa kiasi cha shilingi bilioni
3.1 sawa na asilimia 12.8 ikilinganishwa na shilingi bilioni 21.2 za
bajeti iliyotarajiwa kukusanywa mwaka wa fedha 2011/2012.
Madiwani wameelezea kukerwa kwao na kitendo cha Halmashauri hiyo
kupokea kiwango kidogo cha fedha kutoka serikalini kwa ajili ya matumizi
ya kawaida tofauti na makisio na baadhi ya fedha za miradi ya maendeleo
kutotolewa kabisa na hivyo kukwamisha utekelezaji wa miradi ya
maendeleo katika Halmashauri hiyo.
Post a Comment