HUYU NDIO KIBOKO YA AKINA MESSI NA MULLER - HAYATI GODFREY CHITALU KIBOKO YA MAKIPA WA AFRIKA

HUYU NDIO KIBOKO YA AKINA MESSI NA MULLER - HAYATI GODFREY CHITALU KIBOKO YA MAKIPA WA AFRIKA

Chitalu enzi zake dimbani

Je unadhani Lionel Messi ndio mchezaji ambaye amefunga mabao mengi ndani ya msimu katika historia ya soka la ushindani duniani?

Hapana - kuna jembe kutoka hapo kwa majirani zetu tunaoshea nao reli moja na mabingwa wa Afrika Zambia - ambaye alifunga mabao 107 katika mashindano yote aliyocheza ndani ya mwaka 1972.

Godfrey 'UCAR' Chitalu, ndio mchezaji aliyefanya shughuli hii. Alizaliwa mwaka 1947 na anatajwa kama mchezaji bora wa muda wote nchini Zambia akiwa ndio mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya nchi hiyo.
Makazi ya Milele ya Chitalu


Chitalu ambaye ni mmoja ya watu waliokufa katika ajali ya ndege ya timu ya Zambia iliyotokea mwaka 1993 - aliwahi kuzitumikia klabu za Roan United, Kitwe United, Kabwe Warriors. Pia baada ya kustaafu aliamua kuwa kocha wa timu Kabwe Warriors kuanzia mwaka 1984-1991 kabla ya kupewa majukumu ya benchi la ufundi la timu ya taifa ya Zambia ambayo ndio alikuwa akiiongoza mpaka timu ilipopata ajali ya ndege mwaka 1993 na kufariki dunia.

Pamoja na kuweka rekodi ya kufunga magoli mengi ndani ya msimu mmoja - Chitalu ndio mchezaji aliyefunga mabao mengi ndani ya uzi wa Chipolopolo akiwa na magoli 76 - manne kati ya hayo alifunga kwenye michuano ya kugombea kufuzu katika Olympic 1980 na mechi za michuano yenyewe - ambapo Zambia ilishiriki.

Pia Chitalu ameweka rekodi ya kufunga mabao 11 katika mashindano ya CECAFA - mabao haya aliyafunga katika michuano ya mwaka 1978

Hizi ni baadhi ya rekodi zake nyingine za utunguaji makipa

    •    81 goals  katika mashindano yote mwaka 1968 - in all competitions in 1968(yakiwemo 11  akiwa Zambia)
    •    45 goals in katika mashindano yote mwaka 1969.
    •    51 goals in all competitions in 1971
    •    107 goals in all competitions in 1972
    •    11 goals at CECAFA ’78 which is a CECAFA record


Godfrey Chitalu 
Personal information
Full name Godfrey Chitalu
Date of birth 22 October 1947
Place of birth Luanshya, Northern Rhodesia
Date of death 27 April 1993 (aged 45)
Place of death Gabon
Playing position Forward
Senior career*
Years Team Apps (Gls)
–1967 Roan United

1967–1970 Kitwe United

1970–1982 Kabwe Warriors

National team
1980 Zambia U23

1968–1980 Zambia
(76)
Teams managed
1984–1991 Kabwe Warriors
1993 ZambiaChanzo:- Shaffih Dauda

Post a Comment

Previous Post Next Post