
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA)
Iddi Simba (pichani) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kulitia hasara ya zaidi ya Shilingi
Milioni 300 shirika hilo.
Simba alitinga Mahakamani hapo leo mwenyewe na tuhuma hizo zinamkabili yeye na wenzake wengine wawili wanaotuhumiwa pamoja.
Simba
aliyewahi kuwa Waziri katika awamu ya pili na yatatu anakuwa niWaziri
wa tatu mstaafu kufikishwa Mahakamani hapo kwa tuhuma za kuitia Hasara
Serikali na Mashirika.
Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ilisema hivi karibuni
kuwa, mkataba wa uuzwaji wa hisa za Serikali ndani ya Shirila la
Usafiri Dar es Salaam (UDA) ni batili na kwamba fedha zote zipo kwenye
akaunti ya kada wa Chama Cha Mapinduzi na mwanasiasa wa siku nyingi Idi
Simba, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo na kwa sasa
bwana Simba ni mwenyekiti wa baraza la wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza
muda mfupi na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, baada ya kampuni
iliyodai kununua shirika hilo kutoa taarifa kwa vyombo vya habari mjini
hapa kuhusu ununuzi wa UDA,Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika
ya Umma, Kabwe Zitto alisema ununuzi huo ni batili.
“Niwape
tu ufafanuzi wa jambo hili, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma ndiyo
yenye jukumu la kusimamia sera ya ubinafsishaji, na kwa ufuatiliaji
wetu, tumebaini kuna taratibu za kisheria zimekiukwa, na huyu mtu
anayedai amenunua UDA, afahamu tu kwamba ametapeliwa, UDA bado ni
shirika la umma”,alisema Zitto.
Aliongeza
kuwa kammpuni ya Simon Group inayodai imenunua hisa asilimia 52 ya
shirika hilo, imetapeliwa na kwamba fedha shilingi milioni 300 kati ya
fedha shilingi milioni 760 wanazodai wamesha wekeza kwenye shirika
hili, ziliwekwa kwenye akaunti ya mtu binafsi.
Alisema
fedha hizo zimewekwa kwenye akaunti tofauti ya Idd Simba. Alizitaja
akaunti hizo na tarehe ambazo fedha hizo ziliwekwa, ambapo katika benk M
tawi la Sea View jijini Dar es Salaam, Septemba 2 mwaka 2009, fedha
shilingi milioni 250 ziliwekwa kwenye akaunti binafsi ya Idd Simba .
Aidha, katika benki ya NMB tawi la Makambako, Novemba 26, mwaka 2009 fedha shilingi milioni 30 ziliwekwa kwenye akaunti binafsi ya Idd Simba, na Desemba 9,mwaka 2009 katika benki ya NMB tawi la Mlimani City shilingi milioni 20 ziliwekwa benki na kuingia kwenye akaunti ya Idd Simba tawi la Pride Songea Desemba 18, mwaka huo.
Zitto
alisema kwa uchunguzi wa kamati hiyo kuhusu mwenendo mzima wa
ubadhirifu wa shirika hilo, wamemwagiza CHC kufuatilia shirika la UDA na
kuhakikisha hakuna mali yoyote ya shirika hilo itabadilishwa jina au
kumilikiwa na mtu yoyote bila utaratibu wa sheria za ubinafshishaji.
Chanzo:- Father Kidevu
Post a Comment