Idadi ya watu waliofariki kufuatia mashambulio ya
bomu inazidi kuzua masuali juu ya jukumu la waangalizi wa tume ya Umoja
wa Mataifa nchini humo.
Jukumu lao ni kusimamia na kuona kua mapigano
yanasimamishwa. Lakini ingawa hilo limetimizwa katika baadhi ya maeneo
ukweli ni kwamba mapigano bado hayajamalizika.

Mapigano bado yapo
Na hili linazua suali nyeti juu ya umuhimu na uwajibikaji wa tume ya Umoja wa Mataifa.
Imani iliyokuepo ilikua kwamba endapo watatumwa
wasimamizi kutoka nje huenda wakasaidia kushawishi wakuu wa serikali
kutimiza ahadi zao za kukomesha ghasia.
Lakini tangu mwanzo, kuwepo kwa wasimamizi hawa
kulizua suali jipya kuu: Endapo mashambulizi dhidi ya raia yataendelea
Je nini kitafuata?
Umoja wa Mataifa utachukua hatua gani zaidi ya
hio? Na ni mazingira gani yatafanya Umoja wa Mataifa ukubali kua mpango
wake umeshindwa?
Tatizo ni kua hakukuepo mpango mbadala endapo huu utashindwa.
Mpango pekee ambao Jumuia ya kimataifa uliweza
kukubaliana kwa sauti moja ni huu wa kutuma wasimamizi. Pamoja na maneno
mazuri ya kuvutia ya njia za kupitia kunusuru maisha bila bughdha au
njia nyingine za upatanishi, hakuna yeyote aliyetaka kuhusika moja kwa
moja na matatzio ya Syria.

Makundi yananufaika kwa ghasia
Ingawaje kuhusika kupitia makundi ni njia
nyingine. Bila shaka silaha zimekua zikitiririshwa kutoka nje ya nchi.
Kukiwa na makundi ndani ya nchi ambayo yanafurahia kuzusha fujo kwa
manufaa yao.
Mgogoro wa Syria umeanza kujenga sura ya vita
vya wenyewe kwa wenyewe. Na Umoja wa Mataifa haujajiweka tayari
kutangaza ujumbe wa tume yake umeshindwa kwa sababu hakuna yeyote
anayyeweza kujibu suali - Nini kitafanyika sasa.
Chanzo:- BBC Swahili
Post a Comment