MKUU WA MKOA WA RUKWA AZINDUA UPIMAJI WA AFYA ULIOANDALIWA NA NHIF MKOANI RUKWA LEO
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Injinia Stella Manyanya akipimwa urefu na mtaalamu wa mfuko wa bima ya afya ya
jamii leo katika viwanja vya shule ya Sekondari msakila katika Manispaa ya
Sumbawanga ikiwa ni uzinduzi rasmi wa huduma hiyo ambayo inatolewa bure na mfuko
huo katika kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko pamoja na kujali afya zao.
Shirika hilo lipo katika maadhimisho ya miaka 10 ya utoaji huduma nchini. Katika
hotuba yake fupi Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi
waweze kujua afya zao na kupata ushauri ambao unatolewa bure. Aidha aliwataka
viongozi wa mfuko kutoa elimu ya afya kwa wananchi katika maeneo yote nchini
haswa katika maeneo ya pembezoni kusaidia kupunguza gharama za mfuko
zinazosababishwa na maradhi yanayoweza kuepukika.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
akipima mapigo ya moyo (BP). Vipimo vingine vinavyotolewa ni uwiano wa sukari
mwilini na ushauri bure kwa wananchi watakajitokeza
kupimwa.
Wananchi wengi
wamehamasiku kupima afya zao kama inavyoonekana pichani, rukwareview.blogspot.com (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)



Post a Comment