Taarifa ya SMZ ya matukio ya uvunjifu wa amani

Mohammed Aboud Mohammed, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar.
Aidha, Serikali iliwasihi viongozi hao kuepuka matumizi ya lugha na
vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika nchi yetu na iliwataka
pale ambapo wana maoni yoyote kuhusu serikali wafuate taratibu
zilizowekwa na serikali itakuwa tayari kuzungumza nao ili kuwa na
mustakabali mwema katika nchi yetu. Vile vile, kupitia taarifa maalumu
ya serikali iliyotolewa Aprili Mei mwaka huu serikali ilieleza wazi
kwamba tume ya marekebisho ya katiba imezinduliwa rasmi na kuwataka
wananchi, taasisi na vikundi mbali mbali nchini vyenye nia ya kutaka
kuelimisha umma kuhusu marekebisho ya katiba kufuata muongozo wa sheria
namba 8 ya mwaka jana kama ilivyorekebishwa na sheria namba 2 ya mwaka
huu 2012.
Taarifa rasmi ya serikali kwa wananchi kuhusu matukio ya uvunjifu wa amani nchini
Itakumbukwa kwamba tarehe 25 Aprili, 2012 Kamati Maalumu ya Mawaziri
ilikutana na viongozi wa jumuiya ya Uamsho, Maimamu na Masheikh
kuzungumzia hali iliyojitokeza nchini katika kufanya mihadhara ambayo
ilikuwa inaashiria uvunjifu wa amani.
Katika kikao hicho serikali iliwataka viongozi hao wanapofanya
mihadhara na mikutano inayohusu masuala ya maoni ya katiba wafuate
taratibu zilizowekwa kisheria.
Kwenda kinyuma na sheria hii ni kosa la jinai na hivyo iliwataka
wananchi wote kujiepusha na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na
matakwa ya sheria.
Ndugu wananchi mbali na juhudi hizo za serikali bado wapo watu
wachache wasioitakia mema nchi yetu na umoja uliopo wanaendeleza kwa
makusudi vitendo vya kuvunja taratibu za sheria jambo ambalo limepelekea
jeshi la polisi kuchukua hatua za kisheria.
Ndugu wananchi serikali imesikitishwa na vitendo vilivyojitokeza vya
vurugu na uvunjifu wa amani ambavyo vimeelezwa kwa kina na jeshi la
polisi iliyotolewa mapema leo tarehe 25.05.2012 na kamishana wa polisi
zanzibar.
Kutokana na hali hiyo serikali inawahakikishia wananchi wote kwamba
itaendelea kudhibiti vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria
vinavyoashiria kuondolea nchi yetu amani na utulivu uliopo.
Ndugu wananchi serikali inawahakikishia wananchi kwamba jeshi la
polisi litaendelea kuchukua hatua zifaazo ili kuwahakikishia usalama wa
raia na mali zao unakuwepo na hali inaendelea kuwa shuwari amani na
utulivu.
Ndugu wananchi bado serikali inasisitiza na kuwaomba wananchi wote
waunge mkono juhudi za serikali na kuwacha kabisa kujiingiza katika
vitendo ambavyo vinaashiria uvunjifu wa amani na utulivu katika nchi
yetu.
Hivyo tunawaomba wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida na serikali itaendelea kuwahakikishia usalama wao.
Aidha serikali inawaomba wazazi kuwadhibiti vijana wao wasijiingize
katika vitendo viovu na vurugu kwani jeshi la polisi na vikosi vyote vya
ulinzi na usalama vitakuwa macho kupambana na vurugu hizo na vitendo
vyote vya uvunjifu wa amani.
Kwa madhumuni ya kudhibiti amani na utulivu na usalama wa wananchi wetu serikali katika kipindi hiki itachukua hatua zifuatazo:
1. Inakataza mikusanyiko ya aina mbali mbali, maandamano, na mihadhara ya aina mbali mbali ambayo haijapata kibali cha serikali.
2. Serikali inaliagiza jeshi la polisi kuwatafuta na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika na kufanya fujo zilizotokea katika maeneo mbali mbali ya zanzibar
3. serikali inakemea vikali vitendo vyote vya hujuma na uharibifu wa amali zilizofanywa katika taasisi za umma, dini na mali za watu binafsi.
4. Serikali inawapa pole wananchi na taasisi zilizoathirika na vurugu hizo na kuwahakikishia kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote waliohusika katiak kadhia hiyo.
Na mwisho tunawaomba wananchi kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pale ambapo itaonekana zipo dalili za uvunjifu wa amani katika maeneo yao.

Ahsanteni
Nawashukuru kwa kunisikiliza.
Mohammed Aboud Mohammed, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar.
Chanzo:- www.zanzibaryetu.wordpress.com
Post a Comment