TUMBAKU HUUA WATU MILIONI 6 KWA MWAKA DUNIANI KOTE
NA MWANDISHI WETU
WAKATI Watanzania wakitarajia kudhimisha Siku ya Kutotumia
Tumbaku Duniani kesho, imebainika kuwa tumbaku huua watu takribani milioni
sita (6), kila mwaka.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la
Kumbana na Matumizi ya Tumbaku, Lutgard Kagaruki wakati alipokuwa akizungumza
na wandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam
kuhusu Siku ya Kutotumia Tumbaku Duniani.
Alisema maradhi yabayosababishwa na tumbaku huathiri nchi
zite duniani, na ndiyo maana jumuiya ya kimataifa ikaungana na Mkataba wa
Kimataifa wa Shirika la Afya Duniani wa kudhibiti matumizi ya tumbaku.
Kagaruki alisema Mkataba huo umebeba misingi muhimu ya udhibiti wa matumizi ya
tumbaku, itakayoweza kuokoa maisha ya watu milioni 200 ifikapo mwaka 2050, kama
itatekeleza ipasavyo.
Alisema muingiliano wa kampuni za tumbaku umekuwa tishio
kubwa kuliko yote kwa mikakati ya kutekeleza mkataba wa kimataifa wa kudhibiti
matumizi ya tumbaku.
Kagaruki alibainisha kuwa mkataba huo unavipengele muhimu
kwenye Kanuni namba 5.3 ambacho
kinaeleza bayana mgongano mkubwa wa maslahi uliopo kati ya kampuni za tumbaku
na afya ya jamii
Chanzo:- Full Shangwe

Post a Comment