Utiaji Saini Wizara Miundombinu Zanzibar

Katibu Mkuu wa Wizra ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Vuai Iddi Lila akitia
Saini kwa niaba ya SMZ na Kulia ni Msaidizi meneja Wa Kampuni ya SOGEA ya
Ufaransa kwa kanda Afrika Mashariki Laurent Brouet kwa ajili ya Ujenzi wa Maegesho
na Utanuzi wa Barabara za kutulia na kurukia Ndege katika Uwanja Ndege wa Kimataifa
wa Zanzibar


Talib Ussi Zanzibar

ZAIDI ya b65 Tsh. Zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa Maegesho na utanuzi wa
njia za kurukia na kutua ndege katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Zanzibar
unaojuilikana ‘Abeid Amani Karume International Airport.’
Hayo yameelezwa katika hafla ya utiaji saini kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
na Kampuni ya SOGEA kutoka Ufaransa katika Ofisi za Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano Malindi mjini Zanzibar.
Katika hafla hiyo katibu Mkuu wa Wizara hiyo Vuai Haji Lila alitia saini kwa niaba ya
SMZ na Laurent Brouet ambaye ni msaidizi wa Meneja wa kampuni hiyo kwa kanda
Afrika ya Mashariki ndiye aliyeweka saini kwa niaba ya kapuni yake.
Akifafanua juu ya utiaji saini huo Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano
Zanzibar Issa Haji Ussi alisema pesa hizo ni mkopo kutoka Benki ya Dunia kupitia
Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (IDA) ambazo ziliombwa kwa ajili ya ujenzi huo.

Naibu Waziri huyo alifahamisha kwamba kutekeleza ujenzi huo ni kutimiza mikakati ya
Serikali ya Zanzibar katika kukuza uchumi na kuongeza uingiaji wa Watalii humu nchini.
Alisema kwamba kukamilika kwa ujenzi huo kutapelekea Ndege nyingi kuingia Zanzibar
na wageni kupata nafasi ya kutembelea Nchini jambo ambalo litachochea maendeleo.
“Viwanja vya Ndege ndivyo vinavyotumika sana kwa kuingiza watalii na uwanja wetu
ukikamilika tunatarajia kupokea watalii wengi”alisema Ussi ambaye ni Naibu Waziri.
Ussi alisema mbali na kuongezeka Shughuli za Utalii bali na Wananchi wataweza
kupata ajira nyingi tokea mwanzo wa ujenzi hadi kukamilika na pale utakapoanza kutoa
huduma.
Naibu Ussi alifahamisha ujenzi huo unategemewa kukamilika katika muda wa Miezi 18
na wakandarasi hao watalazimika kukabizi kazi hiyo kwa Serikali ya Mapinduzi kwa
matumizi.
Nae Msaidizi Meneja wa Kampuni hiyo kwa kanda ya Afrika Mashariki Laurent Brouet
alisema atahakikisha Kampuni yake Inakamilisha ujenzi huo kwa wakati huo ambao
umepangwa ili kuondoa Misuguano isiyo yalazima.
“Tutahakiksha ujenzi huu umekamilika kama Mkataba unavyojieleza” alisemanBrouet.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imo katika mikakati ya kuufanya Uwanja wa Ndege
Huo kuwa wa kisasa ili uweze kuruhusu kutua ndege nyingi kwa wakati mmoja.

Post a Comment

Previous Post Next Post