WATU 30 WAPANDISHWA KIZIMBANI ZANZIBAR KWA KUDAIWA KUHUSIKA NA VURUGU NA KUHARIBU MALI
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Watu 30 wakiwemo wanaosadikiwa kuwa
wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam wamefikishwa
katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe wakikabiliwa na makosa
mbalimbali ikiwemo kuwashambulia Polisi,kuchoma moto matairi ya Magali
barabarani na ukorofi.
Mbali na tuhuma hizo,pia wameshtakiwa
kwa kufanya maandamano yasiyokuwa na kibali kinyume na sheria pamoja
na uzembe na ukorofi wa kuwashambuliya polisi kwa mawe.
Watuhumiwa
hao walifikishwa katika mahakama nne tofauti, ikiwemo mahakama ya
hakimu Mohammed Ali Mohammed walikofikishwa watuhumiwa wawili, wanne kwa
hakimu Janet Nora Sekihola, 11 kwa hakimu Omar Mcha Hamza na 11
waliobakia, wamepandishwa mbele ya hakimu Valentine Andrew Katema.
Kwa
nyakati tofauti watuhumiwa hao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya
mikusanyiko isivyo halali, uzembe na ukorofi pamoja kufanya kitendo
kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani.
Watuhumiwa
hao ni Mbarouk Said Khalfani (45), na Mussa Juma Issa (57) wanaodaiwa
kuwa ni viongozi wa read more --->
Jumuiya hiyo, ambapo walifikishwa mbele ya hakimu Mohammed Ali Mohammed, na kusomewa shitaka la kufanya mkusanyiko isivyo halali kinyume na kifungu cha 55 (1) (2) (3) na kifungu cha 56 cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
Jumuiya hiyo, ambapo walifikishwa mbele ya hakimu Mohammed Ali Mohammed, na kusomewa shitaka la kufanya mkusanyiko isivyo halali kinyume na kifungu cha 55 (1) (2) (3) na kifungu cha 56 cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
Wengine
ni Mbwana Hamadi Juma (50), Massoud Hamadi Mohammed (17), Mohammed Juma
Salum (35), Abdulrahman Simai Khatib (19), Hashim Juma Issa (54) Matar
Fadhil Issa (54).
Watuhumiwa
hao kwa upande wao wamefikishwa katika kizimba cha mahakama ya hakimu
Mdhamini Janet Nora Sekihola kujibu shitaka uzembe na ukorofi kinyume na
kifungu cha 181 (d) cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za
Zanzibar.
Wengine
walifikishwa katika mahakama ya hakimu Omar Mcha Hamza na Valentine
Andrew Katema, wakikabiliwa na mashitaka ya kufanya kitendo kinachoweza
kuleta uvunjifu wa amani.
Wakiwa
mahakamani hapo, watuhumiwa hao walishitakiwa chini ya kifungu cha 74
(1) (b) cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
Mashitaka
yote hayo yaliwasilishwa kwa nyakati tofauti na Waendesha Mashitaka,
Wanasheria wa serikali Mohammed Kassim Haasan, Suleiman Haji Hassan
pamoja na Ramadhan Abdallah, kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka
(DPP).
Katika
mahakama ya hakimu Mohammed Ali Mohammed, Mwendesha Mashitaka Mohammed
Kassim alidai kuwa watuhumiwa Mbarouk Said na Mussa Juma, bila ya halali
walipatikana wakiandamana kupitia katika maeneo mbali mbali ya Manispaa
ya mji wa Zanzibar.
Tukio
hilo lilidaiwa kutokea Mei 26 mwaka huu majira ya saa 6:30 za mchana
huko Lumumba wilaya ya Mjini mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, shitaka
ambalo hata hivyo walilikana mahakamani hapo.
Kwa
upande wa watuhumiwa sita waliofikishwa katika mahakama ya hakimu Janet
Sekihola, Mwendesha Mashitaka Suleiman Haji alidai kuwa watuhumiwa hao
walifanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani.
Kwa
mujibu wa Mwendesha Mashitaka huyo, kitendo hicho ni cha kuchoma moto
mipira ya gari barabarani pamoja na kuwarushia mawe askari Polisi, baada
ya kukusanyika isivyo halali katika barabara ya Michenzani wilaya ya
Mjini Unguja, majira ya saa 1:00 za usiku wa Mei 26 mwaka huu.
Katika
mahakama zote hizo, watuhumiwa hao walisimamiwa na Wakili wa
Kujitegemea Abdallah Juma, ambapo aliiomba mahakama hizo kuwapatia
wateja wake dhamana, kwa mujibu wa kifungu cha 150 (1) cha sheria za
mwenendo wa jinai (CPA) namba 7/2004 sheria za Zanzibar.
Watuhumiwa
waliofikishwa mbele ya hakimu Omar Mcha Hamza na Valentine Andrew
Katema, Mwendesha Mashitaka Ramadhan Abdallah kwa nyakati tofauti
aliwasomea watuhumiwa hao mashitaka ya kufanya kitendo kinachoweza
kuleta uvunjifu wa amani.
Wote
hao kwa pamoja walidaiwa kupanga mawe barabarani, kuchoma moto mipira
ya gari barabarani pamoja na kuwarushia mawe askari, kitendo ambacho
kingeweza kuleta uvunjifu wa amani.
Matukio
hayo yametokea Mei 27 mwaka huu, majira ya saa 7:00 za mchana katika
maeneo ya Mfereji wa wima na Amani wilaya ya Mjini Unguja.
Upelelezi
wa mashauri yote hao bado haujakamilika kwa mujibu wa Waendesha
Mashitaka wa mahakama hizo, na kuomba yaahirishwe ili waweze kukamilisha
upelelezi wake.
Mahakama
zote hizo zilikubaliana na hoja hizo za upande wa mashitaka, na
kuziahirisha kesi hizo hadi Juni 11 mwaka huu kwa kutajwa.
Hadi
redio hii inaondoka mahakamani hapo, kulikuwa hakuna hata mmoja
aliyetoka kizuizini, licha ya mahakama hizo kuwapatia masharti ya
dhamana.
Masharti
hayo ni bondi ya shilingi 300,000 na wadhamini watatu waliotakiwa
kusaini bondi ya kiwango kama hicho cha fedha kwa kila mdhamini, ambapo
mmoja kati yao awe ni mfanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Masharti
hayo yametolewa kwa watuhumiwa wawili waliofikishwa mbele ya hakimu
Mohammed Ali Mohammed, ambapo sambamba na masharti hayo wadhamini hao
pamoja na watuhumiwa wenyewe wametakiwa kuwasilisha kopi ya hati ya
kusafiria, barua za Sheha wa Shehia wanazoishi pamoja na kitambulisho
cha Mzanzibari Mkaazi.
Hakimu
Janet Sekihola, Omar Mcha Hamza na Valentine Andrew Katema, kila mmoja
aliwataka watuhumiwa hao kujidhamini kwa bondi ya shilingi 500,000 na
wadhamini wawili wenye vitambulisho watakao wasilisha kiwango kama hicho
cha fedha taslimu, na hakimu Valentine kuongeza kuwa mmoja kati ya
wadhamini hao awe ni mfanyakazi wa SMZ.

Post a Comment