Ajali ya Magari Usiku huu CCM Mbeya kati ya Rav 4 na Fusso. Hakuna aliye umia Dereva wa Fuso akimbia
 Gari la Fusso lililo sababisha Ajali hiyo 
 Namba za gari la Fusso
 Toyota Rav 4 ikiwa imebamizwa vibaya na Fusso hilo 
 Gari la Rav 4 lilivyo haribika kwa nyuma
 Namba za Gari la Rav 4
 Fusso kwa nyuma 
 Fusso kwa Mbele 
***********************************
Ajali Mbaya imetokea usiku huu iiyo husisha Gari la Fusso namba T 596 BUB pamoja na Rav 4 namba 
T 675 ATK, Maeneo ya CCM Mkoani Mbeya. 
Shahidi
 aliye kuwepo eneo la tukio amedai  ya kuwa Dereva wa Gari la mizigo 
Fusso alikuwa mwendo kasi sana, na huku akijaribu kuyapita magari 
mengine matano ambayo yalikuwa mbele yake. Wakati huo anaendelea 
kuyapita magari hayo tayali dereva wa Rav 4 alikuwa amesha washa taa 
kuonesha kuwa anaelekea kulia na ndipo Dereva wa fusso akaligonga Gari 
la Rav 4 ambalo baada ya hapo liliseleleka kwa umbali wa Takribani mita 
300 kutoka usawa wa sehemu ambapo liligongewa. 
Hata hivyo dereva wa Fusso aliyesababisha Ajali hiyo amekimbia eneo hilo. Hakuna aliye umia wala kupata majeruhi.
Chanzo:-  http://mbeyayetu.blogspot.com







Post a Comment