Maafisa wa Nigeria wanasema kuwa ndege ya abiria
imeanguka kwenye eneo la makaazi mengi, katika mji mkubwa kabisa wa
nchi, Lagos.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema waliona ndege ikigonga jengo na kuwaka moto.
Ndege ilikuwa imebeba kama mia-moja-na-50. Haijulikani wangapi wamenusurika.
Mkuu wa Idara inayoshughulika na safari za
ndege, Harold Denuren, alisema ndege hiyo ilikuwa inatoka Lagos, kusini
mwa Nigeria, kuelekea mji mkuu Abuja, kaskazini mwa nchi.
Ndege hio ilianguka katika eneo lililo nje
kidogo mwa uwanja wa ndege.Taarifa ilisema kua wataalamu wa dharura
walikua njiani kufika mahali pa tukio.
Habari zinasema kua hali ya hewa ilikua shuari kukiwa na jua bila sababu ya kusababisha hitilafu.
Nigeria kama Mataifa mengi ya Kiafrika ina
rekodi mbovu ya usalama wa safari za anga, ingawa juhudi kiasi
zimefanywa katika kuboresha hali hio tangu kipindi cha janga la ajali za
ndege mnamo mwaka 2005.
Chanzo:- BBC Swahili

Post a Comment