Kikosi
cha Mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, kimeendelea na
mazoezi jana katika Uwanja wa Kaunda jijini Dar es Salaam,huku miongoni
mwa wachezaji waliosajiliwa msimu huu tayari wakiwa wamejiunga katika
mazoezi hayo.
Katika mazoezi hayo aliyekuwa golikipa wa timu ya Simba Mustapha Ally
Barthez, mshambuliaji wa timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro Said Bahanuzi
na beki wa kulia wa timu hiyo ya Mtibwa Juma Abdul walichangamsha
mazoezi hayo yaliyokuwa yakisimamiwa na Fred Felix pamoja na kocha wa
magolikipa Mfaume Athuman.
Wachezaji wengine walioshiriki katika
mazoezi hayo ni Oscar Joshua,Stephano Mwasika,Nadir Haroub,Ibrahim
Job,Juma Seif,Shamte Ally na Athumani Idd Chuji, wachezaji wengine ni
Omega Seme,Jerryson Tegete,Idrisa Rashid,Godfrey Taita,Nizar
Khalifan,Hamis Kiiza na Kenneth Asamoah.
Wakati huo huo Kocha Fred
Minziro amesema amefurahi kuona kikosi chake kikizidi kuimarika baada
ya wachezaji wengi kujiunga katika mazoezi hayo.
Post a Comment