ABIRIA 65 waliokuwa wanasafiri kwa basi la Kampuni ya Moro Best,
jana walinusurika kifo baada ya basi hilo kuteketea kwa moto katika eno
la Sanga Sanga mkoani Morogoro.
Taarifa zilizotufikia wakati tukienda mitamboni zilisema kuwa, basi
hilo lilikuwa likitoka jijini Dar es Salaam kuelekea Kilombero, na
kwamba chanzo ni hitilafu ya umeme na hivyo kuwaka moto na kuteketea
lote pamoja na baadhi ya mizigo ya abiria.
Hata hivyo, chanzo chetu cha habari kilisema kuwa hakuna abiria yeyote
aliyefariki wala kuumia katika ajali hiyo iliyotokea majira ya jioni na
hivyo, harakati za kuwatafutia abiria usafiri mwingine zilikuwa
zikiendelea.
Kuhusu hali ya usalama ni kwamba Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na
abiria hao waliimarisha ulinzi wa mizigo, na hivyo hakuna upotevu wowote
uliojitokeza kwa mali ziliokolewa.
Post a Comment