BONDIA JAPHET KASEBA AZUNGUMZA NA MO BLOG KUHUSU ‘FREEMASON’.
MO BLOG: Japhet Kaseba
hakuna asiye kufahamu katika ulimwengu wa Tanzania wa mchezo wa Kick
Boxing, hebu tutofautishie kati ya mchezo wa kick boxing unaocheza na
Muay Thai ambayo pia unacheza.
KASEBA: Unajua kick boxing ni staili
ambayo ipo Marekani ambayo inahusisha ngumi na mateke lakini mateke
yake yanaanzia kiononi kuelekea juu, na Muay Thai ni staili kutoka
Thailand ambayo mateke yake yanaanzia kwenye mapaja kwenda juu.
Pia wanatumia Elbow na kushikana na kudondoshana kitu ambacho kwenye kick boxing hakuna.
MO BLOG: Watanzania wategemee nini maana wewe ndie mwakilishi wetu nje ya nchi.
KASEBA: Kubwa ni kwamba baada ya
kukosa wapinzani kwa muda mrefu katika suala zima la Kick Boxing
nikaamua mimi nijiweke pembeni kidogo na kuamua kuanzisha ligi ya
‘Bingwa wa Mabingwa’ kwa Tanzania na baadae Afrika nzima kwa sababu
nilikuwa nakusudia kuwaleta washiriki kutoka Japan na Wanathailend.
MO BLOG: Sasa nini kilitokea na mipango hiyo kukwama..?
KASEBA: Nilikosa udhamini wa kulipia vitu kama sehemu za kulala kwa sababu gharama nyingine walikuwa tayari kujilipia wenyewe.
MO BLOG: Mara ya mwisho tumekujua kama Bingwa wa mchezo wa kick-boxing, lakini ghafla unacheza mchezo wa masumbwi..?
KASEBA: Kama nilivyosema mwanzo baada
ya kukosa mpinzani kwa muda mrefu katika mchezo wa kick-boxing, niliona
ni vyema nikaonyesha kipaji changu katika mchezo masumbwi. Ndipo
nilipopambana na Francis Cheka na mchezo wetu kuharibika baada ya
shabiki kupanda ulingoni.
MO BLOG: Tufafanulie utata uliopo baina yako Francis Cheka katika mchezo wa masumbwi .?.
KASEBA: Kwa mimi binafsi sidhani
kama kuna utata, na kwa sasa najiandaa kwa pambano la marudiano ambalo
nitalitumia kuweka heshima, ambalo litafanyika tarehe 7 mwezi wa 7 ili
kujua nani mshindi wa ukweli.
MO BLOG: Kaseba kuna ukweli wowote kwamba kabla ya kucheza pambano ni vyema siku moja kabla mtu unapaswa kufanya mapenzi.?.
KASEBA: Kwa kweli kwa kuwa mimi
nilianzia kwenye mchezo wa ‘Martial Arts’ , hicho kitu kilikuwa
kinapingwa sana na sidhani hata katika michezo mingine kinakubalika.
Sana sana ningewaasa watanzania kujituma katika mazoezi na kuacha
kudanganyana.
MO BLOG: Hebu izungumzie familia yako kwa sababu mengi yamesemwa na hatupendi kuyarudia.
KASEBA: Nampenda sana mke wangu,
nawapenda ndugu zangu, pia nawapenda sana wazazi wangu na siku zote
namshukuru mwenyezi mungu na naamini hiyo ni moja wapo ya mafanikio
yangu, kwa kuwa kila ninachohangaikia nahaingikia kwa sababu ya familia
yangu.
MO BLOG: Kumekuwa na taarifa kwamba wewe ni Freemason hebu jitetee.!
KASEBA: Ee bwana ehh, ha…ha..ha Mo
Blog mnanizingua lakini nachoweza kusema ni kuwa mimi siwezi kukataa
wala kukubali na waacheni wanadamu waseme wanavyotaka, kwa sababu hata
Kanumba wamesema ni ‘Freemason ‘ lakini najua ni ile ‘movie’ aliyocheza
ndio imemponza.
Upeo wa watu wengi ni mdogo sana, kwa sababu chochote mtu anachokifanya kwa maana ya kuigiza, watu wengi wanaamini ni kweli.
Ndio maana kuna wanawake wameigiza filamu za uchawi na mpaka leo wanaogopwa mitaani wakionekana kweli ni wachawi.
Kwa nchi iliyopo chini kama Tanzania
ambayo inaibukia kila utakachokifanya itaonekana ni hivyo hivyo, hata
ukiigiza ukasema mimi ni rais ndivyo baadhi ya watu watakavyoamini.
Mimi ni mkristo ninayependa kumtumikia Mungu.
MO BLOG: Japhet Kaseba MO BLOG inakutakia mafanikio
katika jitihada zako za kukuza mchezo wa ‘Kick-Boxing’ hapa nchini na
katika kufanikisha ligi ya Masumbwi, na bila kusahau mchezo ujao wa
ngumi kati yako na Francis Cheka; tuko pamoja nawe.
KASEBA: Akhsante sana nami nawatakia kila la heri katika utendaji wenu wa kazi, na msitusahau wanamichezo kama sisi.
SOURCE: dewjiblog.com





Post a Comment