MWENYEKITI WA VILLA SQUAD AJIUZULU UONGOZI WA KLABU HIYO
| Uongozi wa klabu ya Villa na wachezaji. |
Baada ya kufanya
vibaya kwenye ligi kuu msimu uliopita na kupelekea timu hiyo kushuka
daraja, huku mambo yakizidi kwenda ovyo, mwenyekiti wa klabu ya Villa
Squad ya magomeni Dar es Salaam Ramadhani Uledi amejiuzulu kuiongoza
klabu hiyo.
Uledi ambaye aliingia madarakani mwaka jana baada ya kufanyika uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo amejiuzulu kwa kwasababu za kuwajibika. Akiongea na www.shaffihdauda.com Uledi alisema: "Wakati naingia madarakani dhamira yangu kubwa ilikuwa ni kuiwezesha Villa kubaki ligi kuu, lakini nimeshindwa kufanya hivyo, kwa maana hiyo kazi imenishinda. Kwa hiyo ni vizuri kujiuzulu ili kuwajibika, nafikiri sasa kazi hii nimuachie mtu mwingine ili aweze kuliongoza jahazi la Villa na kulirudisha kwenye sehemu nzuri."
Klabu hiyo ya Villa sasa imebakia ikiwa haina uongozi zaidi ya kamati ya utendaji chini Binslum, Ally Kindoile, Mohamed Kimbegele, Hassan Sharif na Moris Simon.

Post a Comment