BAADA ya kufanikiwa kufanyiwa upasuaji wa uvimbe uliokuwa
ukimsumbua mwigizaji na muongozaji wa filamu nchini, Juma Kilowoko
’Sajuki’, imeelezwa kwamba dawa anazozitumia kwa sasa ndizo
zinazomchelewesha kurejea nchini.
Rafiki wa karibu wa msanii huyo, Dennis Sweya ’Dino’, alisema dawa
ambazo Sajuki anazitumia kwa sasa zina nguvu sana kiasi cha kwamba
anatakiwa kuwa chini ya uangalizi maalum wa wauguzi.
Dino alisema kwamba kadiri siku zinavyopita ndivyo Sajuki
anavyoendelea vizuri na akawaomba Watanzania kuendelea kumuombea ili
arudi nyumbani salama.
“Tunashukuru ndugu yetu Sajuki ameshafanyiwa upasuaji na anaendelea
vizuri sana kwa kweli hivi sasa hawezi kurudi kwa kuwa anatumia dawa
ambazo ni lazima asimamiwe na wauguzi lakini hali yake inaimarika kila
kukicha,” alisema Dino.
Alisema kuwa juzi mchana aliweza kuongea na Sajuki mwenyewe kwa simu
na sauti yake ilikuwa yenye kuleta faraja ikiwa imeimarika sana
kulinganisha na wakati alipoondoka.
Sajuki alikuwa katika hali ngumu ya kuumwa kutokana na uvimbe kwenye
ini ambao ulimsababisha kupungua uzito na kutokana na kutokuwa na fedha
za kugharamia matibabu nchini India ilibidi aombe msaada kutoka kwa
wasamaria wema ambao walifanikisha.
Post a Comment