EXCLUSIVE: SELEMAN MATOLA KOCHA MPYA AFRICAN LYON

SELEMAN MATOLA KOCHA MPYA AFRICAN LYON

Hatimaye leo mchana mchezaji wa zamani na nahodha wa klabu ya Simba Selemani Matola amejiunga rasmi na klabu ya African Lyon ya Dar es Salaam kama bosi wa benchi la ufundi.

Matola ambaye pia alikuwa ni kocha wa timu ya vijana ya Simba amejiunga na klabu hiyo ambayo kwenye msimu uliopita ilinusurika kushuka daraja.

Mchezaji huyo wa zamani wa Simba anaenda African Lyon kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na kocha aliyetimuliwa Jumanne Chale ambaye aliiongoza timu hiyo msimu uliopita

Post a Comment

Previous Post Next Post