
Italia na Croatia
SHIRIKISHO la
Soka Ulaya, (UEFA), limeitoza faini ya Euro 25,000 Chama cha Soka
Croatia kwa ghasia zilizozushwa na mashabiki wake wakati wa pambano kati
ya timu yao na Jamhuri ya Ireland.
Mashabiki wa Croatia walirusha fashfash wakati wa mechi hio mjini Poznan iliyomalizika kwa ushindi wa 3-1 jumapili iliyopita.

Mashabiki wa Croatia
Wahudumu wa
uwanja walikabiliana na mashabiki waliovunja uzio na moja kwa moja
kwenda kumbusu Kocha wa Timu ya Taifa Slaven Bilic.
"hukumu hii
imechukuliwa kwa sababu mashabiki waliasha moto na kurusha fashifashi na
mizinga pamoja na kuvamia uwanja,imesema taarifa ya Uefa.
Wakati huo huo
Uefa inachunguza madai kwamba ndizi ilirushwa uwanjani wakati wa mechi
ya kundi C kati ya Italia na Croatia siku ya Alhamisi.
Mpiga picha
mmoja alishuhudia wahudumu wa uwanja wakiokota ndizi na kusikia miliyo
ya nyani iliyoelekezwa mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli.
Croatia itapambana na bingwa wa Dunia na pia wa Ulaya Uhispania katika mechi ya mwisho ya makundi siku ya jumatatu mjini Gdansk.
Ushindi au sare ya 2 - 2 itaiwezesha Croatia kusonga mbele kujiunga na Timu nane zilizovuka hatua ya makundi.
Post a Comment