KABURU: TUNAWASHITAKI YANGA

KABURU: TUNAWASHITAKI YANGA


MAKAMU Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kwamba wataishitaki Yanga kwa kitendo cha kuzungumza na beki wao, Kelvin Patrick Yondan kinyume cha kanuni za usajili.
Akizungumza dakika chache zilizopita, Kaburu (pichani kushoto) alisema kwamba kanuni za usajili haziruhusu klabu kuzungumza na mchezaji wa klabu nyingine bila kupewa ruhusa na klabu yake.
“Kwa mujibu wa fomu tuliyoiona ambayo Yondan amesaini Yanga, wakati anasaini Yanga alikuwa ana mkataba wa miezi sita na Simba, kisheria ni makosa na sisi tutawashitaki kwa kukiuka kanuni za usajili,”alisema.
Inadaiwa Yondan alisaini Yanga, Novemba mwaka jana- wakati ambao wenyewe (Yanga) wanadai alikuwa hana mkataba na Simba SC.
Yondan mwenyewe amekwishakaririwa akikana kusaini Yanga, ingawa fomu ya mkataba imemuumbua leo. Mapema mwezi uliopita Simba ilisema ilikwishaongeza mkataba na Yondan.

Post a Comment

Previous Post Next Post