KAGAME JULAI 14 LIVE ON SUPERSPORT, YANGA KUANZA KUUTETEA UBINGWA - CHAMAZI KUTUMIKA

Mashindano
ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame)
yanayoandaliwa na Baraza la Vyama ya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA) yatafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-29
mwaka huu ambapo timu zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya
Juni 25 mwaka huu.
Yanga
itashiriki mashindano hayo ikiwa bingwa mtetezi, wakati Tanzania Bara
itawakilishwa na mabingwa wake Simba na Makamu bingwa Azam. Mashindano
hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa na Uwanja
wa Chamazi pekee kwa sababu ya kupunguza gharama za uendeshaji.
Ratiba
ya mashindano hayo yanayoshirikisha mabingwa kutoka nchi kumi na moja
ambao ni wanachama wa CECAFA itapangwa Juni 29 mwaka huu.
Mashindano
haya ni muhimu kwa CECAFA na Tanzania Bara ambayo ndiyo mwenyeji kwa
maendeleo ya mpira wa miguu na pia kukuza kiwango cha mchezo huo kwa
ukanda huu ambao kwa Afrika unaoongoza kwa kufanya mashindano mengi ya
timu za Taifa pamoja na klabu.
Mwenyekiti wa
CECAFA ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Leodegar Tenga amewaomba wadau kujitokeza kudhamini michuano
hiyo ambayo itaoneshwa na kituo cha televisheni cha SuperSport. Pia
amewataka washabiki kujitokeza kwa wingi viwanjani kuunga mkono
michuano hiyo.
CECAFA inawashukuru wadau wote kwa
kuwezesha michuano hiyo kufanikiwa akiwemo Rais wa Rwanda, Paul Kagame
kwa kutoa zawadi za fedha kwa washindi, Serikali ya Tanzania kwa kutoa
Uwanja wa Taifa na Kamati ya Utendaji ya TFF kwa kukubali kuwa mwenyeji
wa mashindano hayo.
Chanzo:- Shaffihdauda blog
Post a Comment