Kiungo
wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona Sergio Busquets
ametanabaisha kuwa hakuna hali ya kuelewana kati yake na wachezaji wa
Real Madrid ndani ya kambi ya timu ya taifa ya Hispania. Ikumbukwe kuwa
wiki hii kiungo wa klabu ya Barcelona Xavi alitumia muda mwingi
kuiponda Real Madrid pamoja na kocha wao Jose Mourinho. “Hapa kila mtu
anafanya juhudi kubwa kwa ajili ya timu ya taifa, na kwa matatizo yoyote
yanayojitokeza tunatakiwa tuyaache nje ya uwanja, Kila mchezaji anataka
kuonekana bora. Ni ukweli usiofichika kuwa kuna kipindi inatokea mambo
kutokwenda sawa kutokana na mikwaruzano ya hapa na pale, ila kwa sasa
kila kitu kipo sawa kwani sisi wote lengo letu ni moja. Kiukweli ni
ngumu sana kwa mchezaji kuwa na urafiki na mchezaji mwenzake ambaye
hacchezi klabu moja na yeye hasa kwa zile timu pinzani.”
SIWEZI KUWA NA URAFIKI NA WACHEZAJI WA MADRID - BUSQUETS
Hisia
0
Post a Comment