KOCHA MPYA BARCA ASAINI MIAKA MIWILI NA KUELEZEA MIKAKATI

KOCHA MPYA BARCA ASAINI MIAKA MIWILI NA KUELEZEA MIKAKATI


Tito Vilanova - FC Barcelona
Vilanova

Getty Images
KOCHA mpya wa BarcelonaTito Vilanova leo amesaini mkataba wa miaka miwili na vigogo hao wa Hispania kurithi rasmi mikoba ya Pep Guardiola.
Ilitangazwa Aprili, mwaka huu kwamba wakati Guardiola, aliyeshinda mataji 14 na Los Cules, atakapoachia ngazi kama kocha mkuu, Msaidizi wake huyo, Vilanova atarithi mikoba yake.
Katika Mkutano na Waandidhi wa Habari wa kutangaza kusainishwa kwake mkataba, Vilanova alimshukuru Pep, ambaye alimtambulisha yeye kama mtu aliye tayari kurithi mikoba yake, baada ya kipigo cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kutoka kwa Chelsea.
"Namshukuru Guardiola, rafiki yangu, amekuwa kama kaka yangu. Imekuwa kipaumbele kuwa upande wake kwa miaka mitano," Vilanova alisema kuiambia FCB Live. "Baada ya mechi ya Chelsea, Guardiola aliniambia anataka kupumzika na klabu inaweza kunipa mimi kazi.
Akiwa hajawahi kuongoza timu kabla, Vilanova amesema ataendelea kuomba ushauri kwa Guardiola.
Kocha huyo mpya pia amezungumzia juu ya kufanya mabadiliko kutoka kikosi kilichoachwa na Guardiola: "Mabadiliko? Pep na mimi tunashirikiana kwa kila uamuzi, anawasiliaja nao," alisema. "Hivyo sasa sitafanya mabadiliko mengi. Alves atabaki, hiyo dhahiri. Sielewi tetesi hizo."
Akijibu tetesi za kutengewa bajeti ya kuimarisha kikosi, ambacho kilipokonywa taji la La Liga na wapinzani wao wa jadi, Real Madrid, kocha huyo mpya alikama madai hayo.
"Bajeti ya Euro Milioni 35? Hakuna mtu yeyote aliyeniambia kiwango chochote. Tunataka beki wa kati na wa kushoto. Hatujapanga kusajili mshambuliaji yeyote. Tuna matumaini ya kupunguza idadi ya majeruhi. Cuenca na Tello wapo pia, tuna washambuliaji wa kutosha.

Post a Comment

Previous Post Next Post