Kwa
mujibu wa mtandao wa starcount.com, leo Judith Wambura aka Lady Jaydee
ni mtu wa tatu maarufu zaidi nchini Tanzania kwenye mitandao ya
kijamii.
Mtandao
huo uliozinduliwa rasmi juzi (May 31) ni mkubwa zaidi wa aina hiyo
wenye uwezo wa kusoma tabia za watu bilioni 1.5 duniani kote.
Charts
hizo zinajumuisha mambo yote kuanzia makampuni, wanamichezo,
wanamuziki, vyombo vya habari n.k na kuviweka pamoja kwenye chart ambayo
hubadilika kila siku.
Kwa
leo Jaydee amekamata pia nafasi ya 34 kwa umaarufu mtandaoni kwa
upande wa Afrika Mashariki na kwa dunia nzima amekamata nafasi ya
19,062.
Katika
chart hiyo upande wa Tanzania nafasi ya pili imekamatwa na Hasheem
Thabeet, nafasi ya nne ni mtandao wa Jamii Forums, (5) Mwananchi
Communications, (6) Rais Jakaya Kikwete, (7) Air Tanzania, (8) ZanAir,
(9) Michael Mlingwa, (10) Muhidin Issa Michuzi

Post a Comment