Mbunge: Heri tufe kuliko Muungano

MZIMU wa Muungano umeibuka tena bungeni jana baada ya mbunge wa Micheweni, Haji Khatibu Kai (CUF), kudai kuwa Wazanzibari wako tayari kufa njaa kuliko kuendelea na Muungano aliodai hauna tija.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu, alidai kuwa wananchi wa Zanzibar hawanufaiki na Muungano wakati wanaonufaika ni watu wa upande wa Tanzania Bara.
Mbunge huyo alisema muungano huo umeiondoa Zanzibar katika ramani ya dunia, hivyo ni bora ukavunjwa na kila upande ukaendelea kuwa nchi inayojitegemea.
Hata hivyo, Mbunge wa Magomeni, Muhammad Amour Chomboh (CCM) alitoa taarifa kwa Spika akidai kuwa kinachosemwa na mbunge huyo wa CUF ni mawazo yake.
“Nataka kumpa taarifa mbunge mwenzangu kuwa Wazanzibari ambao ni wazawa na wazalendo wa Zanzibar siyo kweli kuwa wanaukataa Muungano na wala hawako tayari kufa kwa njaa kwa ajili ya kuukataa,” alisema Chomboh.

Post a Comment

Previous Post Next Post