MKATABA KATI YA TANZANIA NA UJERUMANI WASAINI MKATABA
NA MWANDISHI WETU
SERIKALI ya
Tanzania na Ujerumani zimetia saini mkataba ambao utaruhusu wenzi na
wategemezi wa ‘Diplomasia’ kufanya kazi kwenye nchi hizo.
Mkataba huo
umesainiwa jijini Dar es Salaam jana, na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa John Haule, akishirikiana na
Balozi wa nchi hiyo Klaus Peter Brandes.
Haule alisema kuwa, Tanzania ni ya pili kusaini mkataba kama huo, ya kwanza ilikuwa ni nchi ya Zambia.
Vile vile
alifafanua kwamba ingawa Tanzania si mara yake ya kwanza kusaini mkataba
na nchi nyingine lakini inaonesha ni jinsi gani inatambulika ndani na
nje ya nchi hususan katika shughuli za maendeleo.
Aidha,
aliitaja moja ya faida ya mkataba huo ni kuwasaidia watu hao kuendeleza
taaluma zao sanjari na kupanua wigo wa kipato baina ya mtu mmoja pamoja
na familia.
“Kwa sasa
Tanzania imeshaingia mkataba na nchi ya Canada, Marekani, pamoja na
Ujerumani kuna haja ya kushirikiana, ukichukulia kwamba nchi yetu ni
moja ya nchi yenye amani na inatambulika kwa sifa hiyo, hivyo muungano
huu utatuwezesha kufanya kazi kwa uhuru bila kujali huko nchi za
ugeni”alibainisha Haule.
Naye Balozi
wa nchi hiyo Klaus Peter Brandes alisema mkataba huo umeonyesha
ushirikiano mkubwa kati ya nchi hizo mbili, na utaendelea kuleta
mafanikio makubwa kwa siku za mbele.

Post a Comment