Mkurugenzi bodi ya manunuzi kizimbani

Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa mwandamizi wa rasilimali watu wa bodi ya Bodi ya Wataalamu ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB), na mwenzao mmoja jana wamefikishwa katika ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la  matumizi mabaya ya madaraka.

Mwendesha Mashtaka wa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Salha Abdallah aliyekuwa akisaidiana na Sofia Gulla waliwataja washtakiwa hao kuwa ni, Clemence Tesha, Winfrida Igogo na Amani Ngonyani.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Faisal Kahamba, Abdallah alidai kuwa, washtakiwa Tesha na Igogo walitenda kosa la kwanza Juni 22, Mwaka 2010 katika ofisi za PSPTB zilizopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa, siku ya tukio mshtakiwa Tesha akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji na Igogo kama Ofisa mwandamizi rasilimali watu, wakiwa wanatekeleza majukumu yao, kwa makusudi walitumia vibaya madaraka yao kwa kumwajiri Amani Ngonyani katika shughuli za manunuzi kama Meneja Maendeleo wa biashara wa bodi hiyo huku wakijua hakuwa na cheti cha usajili cha wataalamu wa manunuzi kitendo ambacho kilikuwa ni ukiukaji wa sheria.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa, siku na mahali hapo washtakiwa Tesha na Igogo, walimuajiri Ngonyani katika shughuli za manunuzi kama Meneja Maendeleo wa biashara wa bodi hiyo huku wakijua kuwa Ngonyani hakuwa amesajiliwa.

Katika shtaka la tatu, ilidaiwa kuwa siku na mahali hapo mshtakiwa Ngonyani kwa makusudi alikubali kuajiriwa na bodi hiyo katika shughuli za manunuzi kama meneja maendeleao wa bishara katika bodi hiyo wakati akijua kuwa alikuwa hajasajiliwa kama mtaalamu wa manunuzi na ugavi.

Washitakiwa wote wamekana kutenda makosa hayo na wapo nje kwa dhamana baada ya kukidha masharti ya dhamana.
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

Previous Post Next Post