MUDDE ATUA, APEWA JEZI YA YONDAN

MUDDE ATUA, APEWA JEZI YA YONDAN


Mudde

KIUNGO wa kimataifa wa Uganda, Mussa Mudde aliyesajiliwa na mabingwa wa soka Tanzania, Simba SC kutoka Sofapaka ya Kenya, amewasili mchana huu kujiunga na wenzake kuendelea na maandalizi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, imeelezwa.
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga ‘Mr Liverpool’, amesema kwamba, Mudde amewasili na kukabidhiwa jezi ya Kelvin Yondan aliyehamia Yanga na atakuwapo mazoezini jioni hii TCC Chang’ombe, Dar es Salaam.
Mbali na Mudde, pia mshambuliaji wao waliyemsajili kutoka Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny Mrwanda anaanza mazoezi rasmi leo.

Post a Comment

Previous Post Next Post