Meneja wa Sayansi na Uthibiti wa Nestle Tanzania Marsha Yambi (kati) akikabizi zawadi kwa watoto wanaolelewa na kituo cha Chakuwama
Orphanage zawadi ambazo ni moja ya Sehemu ya ushiriki wao katika
kusheherekea siku ya Maziwa Duniani, Pamoja na watoto hao Pembeni ni mlezi wa kituo pamoja na maofisa wakuu wa Biashara Kutoka Kampuni ya Nestle Tanzania.
Mlezi
wa kituo cha Kulea watoto yatima cha Tanzania Mitindo House na
Mwanamitindo Maarufu Bi Khadija Mwanamboka akihojiwa na waandishi wa
habari wakati akipokea zawadi kwa ajili ya kituo cha watoto yatima cha
TMH ambapo Kampuni ya Nestle kupitia bidhaa ya NIDO imewawezesha vituo
vitatu vya watuto yatima vya Dar es Salaam kusherehekea Siku ya Maziwa
Dunia kwa kuwapa Maziwa ya NIDO na Bidhaa za MILO zenye thamani zaidi ya TSZ 5 Milioni.
Bibi Mlezi wa Kituo cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza Bi. Khadija akifafanua jambo wa waandishi wa habari juu
ya Changamoto anazozipata katika harakati za uendeshaji wa Vituo vya
watoto yatima pamoja na Michango ya Taasisi mbalimbali kama Kampuni ya
Nestle NIDO ilivyofanya kuwawezesha watoto kuwa na afya bora na
kuhamasisha Unywaji wa Maziwa halisi ya Ng’ombe yaliokatika mifumo mbali
mbali.
Bidhaa za NIDO, CereVita, MILO kutoka Kampuni ya Nestle Tanzania zenye thamani ya TZS 5,548,800 Zilizogawiwa kwa vituo vyam kulea watoto yatima vya Umra, Chakuwama na Tanzania Mitindo house jijini
dar es salaam zenye watoto takribani 200 wanaolelewa na vituo hivyo
katika kuazimisha siku ya Maziwa Duniani ambayo hufanyika kila mwaka
Juni 1st.
Chanzo:- Father Kidevu( http://mrokim.blogspot.com)
Post a Comment