KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan amethibitisha rasmi
kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea Yanga na kuahidi
kushirikiana vema na Haruna Niyonzima na Juma Seif kuipa timu hiyo
mafanikio.
Wakati Khalfan akizima minong'ono iliyotawala hapo kabla kuwa amejiunga na Simba, naye nahodha wa mabingwa hao wa Kombe la Kagame, Shadrack Nsajigwa amesema hatalazimisha kupewa mkataba mpya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Khalfan alisema ameamua kujiunga na Yanga akiamini ni klabu imara na inayoweza kutimiza matarajio yake.
"Hakuna sababu ya kuficha tena, mimi na Yanga tumemalizana, kifupi ni kwamba nimesaini mkataba wa mwaka mmoja," alisema Khalfan na kuongeza kuwa:
"Kimsingi nafurahi kucheza pale kwa sababu Yanga ina wachezaji wazuri, napenda kucheza pamoja na Haruna Niyonzima kwani naamini ushirikiano wetu utatoa matokeo mazuri na hata Juma Seif namfahamu nilipata kucheza naye."
Akizungumzia ni jinsi gani anauchukulia ushindani wa namba, Khalfan alisema anakubaliana na changamoto ya aina hiyo kwa sababu inamsaidia mchezaji asibweteke na badala yake ajitume wakati wote.
"Jaribu kufikiri katika kazi yoyote kama hakuna ushindani nini kinatokea ni lazima utajisahau na hauwezi kupiga hatua, kwa upande wangu mazingira ya namna hii ndiyo nayapenda kwa kuwa yananipa changamoto na kunifanya nijitume wakati wote,"alisema Khalfan.
Kabla ya kusaini Yanga, Khalfan aliwahi kuzichezea timu za Al Tadamol ya Kuwait, Vancouver Whites Caps na Philadephia Union zinazoshiriki Ligi Kuu ya soka ya Marekani (MSL).
Katika hatua nyingine nahodha wa Yanga aliyemaliza mkataba wake, Shadrack Nsajigwa amesema hawezi kulazimisha kuongezewa mkataba na klabu hiyo.
Nsajigwa alisema kuwa hawezi kuwaomba wamuongezee mkataba kama watafanya hivyo sawa, lakini hawezi kuwapigia magoti.
"Sijawahi na siwezi kufanya kitu kama hicho yaani niombe kuongezewa mkataba...siwezi," alisema Nsajigwa.
Wakati Nsajigwa akisema hayo habari zilizopatikana jana jioni zilidai kuwa Nsajigwa ni kati ya wachezaji walioko katika orodha ya watakaotema wakiwamo mshambuliaji Davis Mwape
Wakati huohuo; Klabu ya Azam imelalamikia kitendo cha Simba kutaka kumsajili chipukizi wao Ibrahim Rajabu Jeba bila ya kufuatwa utaratibu.
Jeba anayecheza timu ya vijana ya Azam chini ya miaka 20 alionekana akifanya mazoezi ya gym na wachezaji wa timu ya Simba.
Akizungumzia suala hilo Meneja wa Azam, Patrick Kahemela alisema Jeba ana mkataba wa miaka minne wa kuitumia klabu hiyo hivyo kwa yeyote anayemuhitaji hana budi kukutana na uongozi wa Azam na si kumchukua kwa njia za panya.
"Tunajua Simba wameanza kumrubuni Jeba tangu Januari, lakini kama na sisi tutaamua kufanya hivyo kwa wachezaji wao sidhani kama kutakuwa na maelewano baina yetu,"alisema Kahemela.
Kahemela aliongeza kuwa mchezaji huyo ni mchezaji wao halali na waliingia mkataba naye tangu mwezi Desemba na hawatakaa kimya wala kumuachia aende hivi hivi bila ya kuchukua hatua za kisheria.
Katibu Mkuu wa Simba, Evodus Mtawala alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema haelewi nini kinaendelea ingawa amesikia habari kama hizo na kuahidi kutolea ufafanuzi kesho.
"Siwezi kukurupuka kutoa majibu nafanya uchunguzi na nitalitolea ufafanuzi Jumanne kwa kuwa kwa sasa sina taarifa rasmi kuhusu jambo hilo na mimi nimesikia tu kwenye vyombo vya habari,"alisema Mtawala.

Post a Comment