MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi ameibuka shujaa wa Uganda Cranes
baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Angola katika mchezo wa
kufuzu kwa Kombe la Dunia 2014 uliofanyika jijini Luanda.
Wenyeji Angola walipata bao la kuongoza mapema katika dakika ya saba lililofungwa na Campos Braume Manuel Abel Djalma.
Uganda
ilipata nafasi za kusawazisha bao hilo, lakini washambuliaji wake Mike
Serumaga na Martin Mutumba walishindwa kutumia nafasi hizo walizozipata.
Zikiwa
zimebaki dakika tano mchezo kumalizika kikosi cha Bobby Williamsons
kilionekana kupotea kabisa mchezo ndipo Okwi alipokea mpira na kupiga
shuti lililojaa nyavuni katika dakika ya 88.
Bao hilo la Okwi siyo
tu limeinusuru Uganda na kipigo, lakini limeipa Cranes pointi moja
muhimu katika jiji la Luanda na kushika nafasi ya pili Kundi J nyuma ya
Senegal watakayopambana nayo wiki ijayo.
Post a Comment