Ouattara waasi Afrika washughulikiwe

RAIS wa Ivory Coast,  Alassane Ouattara, amezitaka nchi za Afrika, kuwa na mikakati ya pamoja ya kukabiliana  tatizo la makundi ya waasi yanayochangia vita katika mataifa ya Afrika na hivyo kuathiri uchumi wa bara la Afrika.

Akizungumza katika mkutano  wa  mwaka wa 47 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB), unaonendelea mjini Arusha,  Ouattara alisema ni muhimu kuwa na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha kuwa nchi zaAfrika, zinakuwa na utawala wa kidemokrasia na kuzuia waasi kusambaratisha uchumi wa nchi hizo.
Rais Ouattara pia alisema nchi za Afrika hasa ya Kaskazini, zinakabiliwa na tatizo la athari za tabianchi inayotishia usalama wa chakula.

Alisema ukame unaotokana na mabadiliko ya tabianchi, unaathiri mno uzalishaji wa mazao ya chakula na kwamba kuna haja ya kushirikiana ili kukabiliana na tatizo hilo.

Ouattara alisema, usalama wa chakula barani Afrika ni moja ya mambo yanayopaswa kuwekewa mkakati madhubuti ili kuhakikisha kuwa Afrika ina kuwa na uwezo wa kujitosheleza kwa chakula kwa wakati wote na hata kuuza nje ya bara.

Kiongozi huyo pia alisema kuna haja ya kupambana na tatizo la uharibifu wa mazingira na kuongeza uwekezaji katika sekta ya kilimo katika nchi nyingi.

Wakati huo huo,Morocco,  imeunga mkono uamuzi wa fDB, kufanya mkutano ujao katika nchi na kwamba itajipanga ili kuhakikisha kuwa mkutano huo unafanyika kwa mafanikio makubwa.

Akizungumza katika mkutano huo jana, Mwakilishi wa Mfalme wa Mohammed  Morocco,  alisema taifa hilo  lipo katika mikakati ya kuboresha uchumi na demokrasia na kufanyika mkutano huo.

Katika mkutano huo, pia rais mtaafu Botswana, Festus Mogae na mabalozi wa nchi mbalimbali wanashiriki  na hadi jana wajumbe 2,400 ndio walikuwa wamejiorodhesha kwa mkutano huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post