Producer wa hits kadhaa za
bongo kama Mama ntilie na ni Wewe ya Amini, pamoja na umaarufu wake
kuzidi kukua every day, amesema kuna vikwazo anavyovipata kwenye kazi
hasa kutoka kwa baadhi ya wasanii.
C 9 amemtaja mwimbaji Linex kwamba ndio msanii namba moja alie msumbua na kumkwaza.
Amesema “wasanii wengi ambao
wanazingua lakini binafsi naweza kumzungumzia mtu kama Linex kwa sababu
imeniumiza kidogo, nakumbuka tulifanya nae bure ngoma ya Ngekewa na
baadae tukafanya ngoma yake nyingine na Diamond for free lakini baadae
alikuja kufanya ngoma nyingine ambayo alikwenda kuirudia sehemu
nyingine, kabla ya hapo tulimwambia alipie hiyo ya mwisho ili kuchangia
gharama za studio kidogo ndio akakimbia”
Kwenye line nyingine C-9
amesema “baada ya kumwambia hivyo alikimbia ndio tukaja kusikia
amekwenda kuirudia na kuifanyia video sehemu nyingine, hajafanya kitu
kizuri kwa sababu kama angetaka kurudia angeniambia tu, alafu sababu
nyingine inayomfanya Linex asirudi tena Kiri Records ni yeye kupoteza
simu yangu ambayo kila nikimdai anaanza kuwaka… Ohhh mbona tunasumbuana
mwanagu simu tu unataka tukosane? hivyo ndio anavyosema
Chanzo:- http://millardayo.com

Post a Comment