SIMBA YAACHANA NA DANNY MRWANDA, NYOSO ALETA POZI
MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Simba wamefuta
mpango wa kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wao Dan Mrwanda (Pichani) anayecheza soka la
kulipwa katika klabu ya DT Long An ya Vietnam, imfahamika.
Mmoja ya viongozi wa Simba alisema jana
kwamba, wameamua kuachana na Mrwanda kufuatia masharti aliyewapa, sambamba na
dau la shilingi Mil.12 alilolitaka ili kuweza kumwaga wino.
“Tumeamua kuachana na Mrwanda kwani pamoja na kutaka dau la
mil.12, pia ametaka mkataba atakaousaini umruhusu kwenda nje iwapo atapata timu
ya kuichezea, kitu hicho hatukubaliani nacho kwani ni sawa na kutupa
fedha,”alisema kiongozi huyo.
Kama hiyo haitoshi,
kiongozi huyo aliongeza kuwa bado wapo katika majadiliano juu ya kuongeza
mkataba wa beki wao Juma Nyoso ambaye ameonekana kuvimba kichwa baada ya
kuondoka kwa Kelvin Yondan, hivyo kutaka aongezewe dau.
Katika hatua nyingine, baadhi ya wachezaji wa timu hiyo
wakiwemo nyota wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi
na michuano ya kimataifa wameanza mazoezi

Post a Comment