CAIRO, MisriMABINGWA wa Afrika, Zambia wamekubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Sudan, huku Ivory Coast na Senegal wakianza kwa kishindo kampeni zao za kusaka kufuzu kwa Kombe la Dunia 2014.
Zambia iliyoifunga na Sudan katika robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2012, lakini hali haikuwa hivyo juzi Jumamosi usiku hali iliyosababisha kocha wao Mfaransa, Herve Renard kusema kufungwa huko kumetokana na wachezaji kubweteka.
Wenyeji Sudan wakiwa jijini Khartoum walianza mchezo huo wa Kundi D kwa kasi na kutawala mechi hiyo kuanzia mwanzo hadi mwisho na kufanikiwa kupata mabao katika kipindi cha pili kupitia Mohamed Tahir na Saifeldin Ali.
Kocha Renard anayelipwa mshahara wa kiasi cha dola 100,000 kwa mwezi kwa lengo la kuhakikisha Chipolopolo inafuzu kwa mara ya kwanza kucheza Kombe la Dunia alitadhalisha kabla ya kuelekea Khartoum.
"Ninauhakika sisi si timu bora Afrika ...
kuna timu nyingine ni bora zaidi yetu na tunajua hilo ... tunatakiwa
kuwa bora, bora zaidi ili tufuzu kucheza Kombe la Dunia," aliimbia BBC.
Pamoja na kipigo hicho bado safari ya Zambia itakutana na kingingi kingine hapo Juni 9, mbele ya Ghana, ambayo ilisambaratisha Lesotho 7-0 siku ya Ijumaa.
Jijini Abidjan, mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Sabri Lamouchi aliyechukua mikoba ya kuiongoza Ivory Coast wiki hii, pamoja na kukosa uzoefu wa kazi hiyo amefanikiwa kuiongoza nchini hiyo kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wachezaji 10 wa Tanzania.
Mabao ya Tembo hao yalifungwa na Salomon Kalou na Didier Drogba huku beki wa Tanzania, Aggrey Morris akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi mbili za njano.
Senegal walioshindwa kutamba kwenye fainali za Mataifa ya Afrika 2012 kwa kufungwa mechi zote tatu za hatua ya makundi, waliruhusu bao la mapema na Liberia jijini Dakar pamoja na mshambuliaji wa Newcastle United, Papiss Demba Cisse akikosa penalti.
Lakini Simba hao wa Teranga Lions walituliza presha ya kocha wao wa muda Joseph Koto kwa kusawazisha bao hilo kupitia Ibrahima Balde kabla ya Dame Ndoye na Sadio Mane kufunga mabao mengine kwenye kushinda 3-1, na kuongoza Kundi J.
Morocco walilazimisha sare 1-1 nyumbani dhidi ya Gambia baada ya Houssine Kharja kusawazisha bao la mapema la beki Abdou Jammeh wa wagenini.
Tunisia walilazimika kusawazisha kabla ya kupata ushindi wake wa mabao 3-1 dhidi ya Equatorial Guinea mjini Monastir, Sierra Leone ilichapa Cape Verde Islands kwa mabao 2-1 jijini Freetown nao Burkina Faso wakiwa mjini Ouagadougou walilazimishwa kwenda suruhu Congo Brazzaville.

Post a Comment