USAJILI wa Danny Mrwanda
katika klabu bingwa ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa
2011/2012 Simba, umezua jambo baada ya kamati ya ufundi ya
klabu hiyo kutokubaliana nao.
Awali nyota huyo aliyewahi kukipiga
Simba kabla ya kutimkia katika klabu ya DT Long An ya Vietnam,
aliomba kusajiliwa tena Simba kwa masharti maalum lakini kamati ya ufundi ya
Simba chini ya Mwenyekiti wake Ibrahim Masoud ‘Maestro’ ilipinga.
Habari kutoka Simba zinaeleza
kuwa Mrwanda alitaka asajiliwe kwa dau la shilingi milioni 12 huku pia mkataba wake umruhusu kwenda katika
timu yoyote atakayoipata nje ya nchi,kitu ambacho kilipingwa na kamati ya
ufundi.
Hata hivyo pamoja na kamati
ya ufundi ya Simba kupinga usajili wa mchezaji huyo, makamu mwenyekiti wa klabu
hiyo Geofrey Nyange ‘Kaburu’ aliamua kumsainisha mkataba mshambuliaji huyo.
Mmoja ya viongozi wa Simba
ambaye hakupenda kutajwa jina lake mtandaoni alisema
wanasikitishwa na kitendo kinachofanywa na Kaburu kwani kamati ya ufundi ndiyo
inajua ubora au udhaifu wa mchezaji sambamba na mapungufu yaliyopo ndani ya
timu.
Alisema hali hiyo imekuwa
ikijitokeza mara kwa mara na matokeo yake wengi wa wachezaji ambao wamekuwa
wakisajiliwa ‘kimabavu’ wameshindwa kutoa mchango wowote ndani ya timu hiyo.
“Ndiyo tunajua Kaburu ana
nguvu na uwezo mkubwa katika timu lakini kwa nini aingilie kazi za kamati ya
ufundi,kama ni hivyo hakukuwa na maana ya
kuwepo kwa hiyo kamati,”alisema mtoa habari huyo.
Post a Comment