Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama chupa ya chai ya mti katika kilele cha
sherehe za kutoa ruzuku kwa wajasiliamali waliofanya vizuri katika
Progamu ya fanikiwa kibiashara zilizofanyika kwenye viwanja vya Mbazi
mmoja jijini Dar es salaam juni30,2012.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji, Dkt, Mary Nagu.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia moja kati ya viatu vilivyoonyeshwa
kwenye banda la Mareshi Shoe Maker katika kilele cha sherehe za kutoa
ruzuku kwa wajasiliamali waliofanya vizuri katika Progamu ya fanikiwa
kibiashara zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es
salaam Juni 30,2012.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji, Dkt, Mary Nagu na kulia Mwenyekiti wawa
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Mama Ester Mkwizu. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka wajasiriamali wa kati na wadogo
nchini wawe waangalifu na makini katika biashara wanazopanga kuzifanya
kama kweli wanataka kufanikiwa maishani na akawaonya wale waliopata
mbegu mtaji kuchukua tahadhari zaidi.
Ametoa onyo hilo leo mchana (Jumamosi, Juni 30, 2012) wakati
akizungumza na wajasiriamali kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na
Visiwani ambao walihudhuria sherehe za kutoa zawadi kwa washiriki wa
Programu ya Fanikiwa Kibiashara (Business Development Gateway - BDG)
kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
“Naomba
niwatahadharishe kuwa ujasiriamali unataka umakini wa hali ya juu.
Mmoja wa Wajasiriamali mashuhuri huko Marekani aliwahi kutoa tahadhari
kwa kusema: "Business is like oil, it won't mix with anything but Business" akimaanisha kwamba biashara ni kama mafuta ya kulainisha mitambo (oil) ambayo hayachanganywi na kitu kingine chochote, isipokuwa oil yenyewe. Tunahitaji uangalifu na umakini katika kufanya biashara zetu bila kuchanganya na mambo mengine
Amesema mtu anapochukua mkopo kwa nia ya kuanzisha biashara kisha
akaamua kuoa mke wa tatu au kununua gari kwa kutumia fedha hiyo ya mtaji
ni lazima atakwama kwa sababu atakuwa amechakachua dhima nzima ya ile
biashara yake.
Alisema katika mabanda ya maonesho aliyotembelea leo, ameona changamoto
kuu tatu ambazo zinahitaji kuangaliwa haraka ili kuinua soko la bidhaa
za wajasiriamali hao.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa vifungashio bora, ukosefu
wa alama za viwango kutoka shirika la viwango nchini (TBS) na ukosefu wa
alama ya biashara (bar code) katika bidhaa zao. “Bidhaa zenu ni lazima
ziwe na vifungashio vizuri vyenye mvuto ili mnunuzi ashawishike
kununua.”
“Nawasihi mfuate masharti ya shirika la viwango nchini ili bidhaa zenu zikubalike, waoneni wahusika ili mpate bar code kwenye bidhaa zenu. Bidhaa zenu zikiwa na bar code zitakubalika kokote ulimwenguni,” alisisitiza.
Waziri Mkuu pia alisema anatatizwa na changamoto moja kuu ambayo ni ya
kuhakikisha mpango wa BDG unaendelezwa ili uwanufaishe watu wengi zaidi.
“Mpango huu umefikia mwisho, na umedumu kwa miaka minne tu. Mwenyekiti
wa TPSF itabidi tuangalie hata uwezekano wa kukopa ili jambo hili zuri
lisiishie hapa,” alisema.
Post a Comment