WELBECK AING'ARISHA ENGLAND
MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Danny Welbeck ameifungia bao lake la kwanza timu ya taifa ya England, wakati kikosi hicho cha Roy Hodgson kikiibuka na ushindi wa 1- 0 dhidi ya Ubelgiji katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na Euro 2012 kwenye Uwanja wa Wembley.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 21, amejiwekea mazingira ya kuanzishwa kwenye
mechi ya kwanza ya Euro dhidi ya Ufaransa Jumatatu kwa bao lake hilo
tamu kipindi cha kwanza.
Post a Comment