Yanga yanasa wawili

 Yanga yanasa wawili

JUMA Abdul amesema tayari amemwaga wino ili kuvaa jezi za rangi ya Njano na Kijani msimu ujao wa Ligi Kuu Bara. Anajiunga na klabu hiyo ya Jangwani akitoka Mtibwa Sugar.
Na kauli yake ya ziada wakati akichekelea kutia saini mkataba wa kuichezea Yanga, ilikuwa: "Nimekuja Yanga kuwapa furaha mashabiki."
Abdul alisema hana cha kuficha, kwani tayari ameshamalizana na Yanga.
"Nitavaa jezi za Yanga msimu ujao, nimesaini mkataba wa miaka miwili," alisema Abdul.
"Kupata fursa ya kucheza timu kubwa kama Yanga ni hatua kubwa ya maendeleo kwangu, natumaini nitafanya kile ambacho Yanga wamekipenda toka kwangu," alisema.
"Ninachoahidi kwa mashabiki wa Yanga ni kuwataka watulie, nimekuja kufanya kazi na hawatajutia usajili wangu."
Katika hatua nyingine, mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Said Bahanuzi jana alitarajia kusaini mkataba na Yanga
Mchezaji huyo alitarajia angesaini mkataba mapema, lakini ilishindikana baada ya kuingia mkataba mpya na Mtibwa baada ya ligi kumalizika.

Post a Comment

Previous Post Next Post