MABINGWA wa Ligi ya Mabingwa, Chelsea na Manchester United zimeanza vema
ziara zao kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Seattle Sounders ya Marekani
na AmaZulu ya Afrika Kusini.Chelsea ikiwa ziarani nchini Marekani ilichapa Seattle Sounders kwa mabao 4-2, huku Manchester United ikipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya AmaZulu ya Afrika Kusini.Mshambuliaji chipukizi wa Ubelgiji, Romelu Lukaku alifunga mabao mawili kabla ya nyota wapya wa Chelsea, Eden Hazard na Marko Marin nao kufunga bao moja kila moja katika ushindi huo wa Jumatano usiku.
Mshambuliaji Lukaku alifunga bao la kwanza dakika ya tatu na bao lake la pili alifunga dakika 44 ya kipindi cha kwanza.
Seattle waliamka na kusawazisha mabao hayo kupitia Fredy Montero kabla ya chipukizi wapya wa Chelsea kutulia na kuongeza mabao mengine mawili yaliyofungwa na Hazard, aliyepiga shuti lililomgonga beki Jhon Kennedy Hurtado na kumchenga kipa Bryan Meredith na kujaa wavuni.
Naye Marin aliyetegeneza mabao mawili ya kwanza kwa Chelsea alifunga bao la nne dakika 85 kwa shuti lake kumgonga Parke na kujaa wavuni.
PRETORIA;
Manchester United imeanza ziara yake ya michezo sita duniani kwa
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AmaZulu mbele ya mashabiki 50,000
waliojitokeza kwenye Uwanja wa Moses Mabhida juzi.Federico Macheda alifunga bao hilo pekee dakika ya 20, akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Paul Scholes na Dimitar Berbatov.
Matokeo hayo yameokana kuwashangaza watu wengi wa Afrika Kusini kuona timu ya AmaZulu iliyomaliza katikati msimamo wa ligi kuwazuia mabingwa hao wa zamani wa Ulaya waliocheza bila ya nyota wake kama Wayne Rooney.
Mwanasiasa mkongwe Nelson Mandela, na rais wa kwanza wa Afrika Kusini aliyepatikana kwa kupigiwa kura na wote alipongezwe kabla ya mchezo wa kutimiza miaka 94 ya kuzaliwa kwake.
"Wachezaji wangu walichoka katika kipindi cha pili," alisema kocha wa United, Sir Alex Ferguson. "Nimefurahi kwa kupata ushindi huu ambao ni zawadi tosha ya kumpa Nelson Mandela katika siku yake ya kuzaliwa.
"Nilitoa nafasi kwa vijana wengi usiku huu na tuna matumaini wawili au watatu wataingia kwenye kikosi cha kwanza. Jesse Lingard ameonyesha uwezo mkubwa kama ilivyokuwa kwa Scott Wootton aliyecheza vizuri kwenye ulinzi."
Kiungo mpya wa United, Shinji Kagawa alikuwa benchi kabla ya kuingia dakika moja kabla ya mpira kumalizika.
Katika mchezo huo United ilianza na beki wake mkongwe Rio Ferdinand na chipukizi Robbie Brady, Frederic Veseli, Wootton na Lingard kwenye safu ya ulinzi
Kesho Manchester United itacheza dhidi ya Ajax Cape Town kabla ya kukwea pipa kuelekea China watakapokuwa na mechi katikati ya wiki ijayo dhidi ya Shanghai Shenhua, klabu iliyomsajili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba.
Klabu hiyo ya Old Trafford itakuwa na mechi dhidi ya Valerenga nchini Norway, pia itaivaa Barcelona huko Sweden na kumaliza na Hanover ya Ujerumani katika kumalizia safari yake ya kuzunguka dunia ya kilomita35,400 kabla ya kuanza kwa kampeni zake za Ligi Kuu dhidi ya Everton.
Post a Comment