DOKTA SLAA AJISALIMISHA MIKONONI MWA POLISI!!

DOKTA SLAA AJISALIMISHA MIKONONI MWA POLISI!!

Baada ya kutamka hadharani kupitia vyombo vya habari kuwa usalama wa taifa unapanga mipango ya kuwauwa viongozi wa juu wa Chadema akiwemo yeye Dokta Slaa na Mbunge wa Ubungo Ndugu John Mnyika na baadaye kugoma kwenda polisi kutoa uthibitisho wa kauli hiyo alipotakiwa afanye hivyo na jeshi la polisi sasa Dokta akubali kufika polisi. Picha juu ni kiongozi huyo wa Chadema akishuka kutoka kwenye gari lake punde
alipowasili makao makuu ya polisi jijini Dar Es Salaam kutii amri ya kutoa uthibitisho wa kauli alizozitoa siku kadhaa zilizopita juu ya Njama za usalama wa taifa kutaka kuwaangamiza viongozi hao amri ambayo hapo mwanzo Dokta aligoma kwa kile alichodai kuwa hana imani na jeshi la polisi nchini.

Picha juu ni Dokta slaa akisalimiana na baadhi ya wafuasi wa Chadema waliofika makao makuu kujua kinachoendelea, Pembeni yake ni aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini Ndugu Godbless Lema.

Post a Comment

Previous Post Next Post