Ghasia zimeongezeka Syria-UN

Kambi ya wanajeshi walioasi nchini Syria
Kambi ya wanajeshi walioasi nchini Syria
Afisa mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na haki za kibinadam Navi Pillay ameonya kuwa viwango vya ukiukwaji wa haki za kibinadam vinaendelea kuongezeka nchini Syria.
Pillay, amesema ghasia nchini Syria, zinaendelea kuchochewa na kuongezeka kwa idadi ya silaha miongoni mwa wanajeshi wa serikali na upinzani.
Hatab hivyo Bi. Pillay, hakusema mahala ambako silaha hizo zinatoka lakini waandishi wa habari wanasema serikali ya Syria, inapokea msaada wa silaha kutoka kwa serikali za Iran na urusi.
Upinzani nao ukipewa silaha na serikali za Qatar na Saudi arabia.
Awali Muungano wa nchi za Kiarabu, ulitoa wito kwa upinzani kuungana na kuafikiana kuhusu mpango kwa kipindi cha mpito nchini humo.
Kiongozi wa Muungano huo, Nabil Al Arabi, ameliambia kongamano la wanaharakati wa upinzani mjini Cairo, Misri, kuwa Syria, inahitaji mfumo wa Kidemokrasia ambao hautabagua mtu yeyote.
Wakati huo huo, vyombo vya habari nchini Uturuki, vimesema kuwa wanajeshi 85 wa syria wakiwemo generali mmoja na maafisa wengine 7 waandamizi wamevuka mpaka na kuingia nchini humo.
Mashirika hayo ya habari yametaja kundi hilo kama kubwa zaidi la kijeshi ambalo limeasi na kuingia nchini Uturuki tangu machafuko ya kisiasa kuanza nchini Syria.
Kundi hilo linaripotiwa kutumwa katika kambi moja ya wakimbizi Kusini mwa Uturuki.
Wiki iliyopita, kundi lingine la ziadi ya wanajeshi 30 na familia zao wakiwemo maafisa kadhaa wakuu walivuka mpaka na kuingia Uturuki.
Chanzo:- BBC Swahili

Post a Comment

Previous Post Next Post