KIVYOVYOTE NATAKA KOMBE - STEWART HALL(KOCHA AZAM)
![]() |
| Stewart Hall |
Kocha wa Azam FC, Muingereza Stewart
Hall amesema kwamba Yanga ni timu nzuri na fainali ya Klabu Bingwa ya
soka Africa Mashariki na Kati itakuwa ‘classic’, yaani baab kubwa kesho
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Stewart ambaye mapema mwaka huu
aliiwezesha Azam kutwaa taji la kwanza, Kombe la Mapinduzi, alisema
kwamba Yanga imekuwa ikiimarika siku hadi siku na sasa imefikia kuwa
timu bora na anatarajia upinzani mkali kesho.
Akizungumza baada ya mechi za Nusu Fainali jana, Muingereza huyo alisema kwamba pamoja na ukweli huo nia yao Azam ni kutwaa Kombe hilo.
“Vijana wangu hadi sasa wamenifurahisha
kwa kucheza kwa kufuata maelekezo yangu. Mechi na AS Vita ilikuwa ngumu,
hadi mapumziko tulikuwa nyuma kwa 1-0. Lakini niliwaambia tukiwa
vyumbani, watulie tuendelee kucheza mpira wetu, tusihamaki, walinielewa
na wakacheza nilivyotaka.
Hiyo ndio siri ya ushindi, kwa kiwango
kile na uchezaji ule, naona kabisa tunaweza kuwafunga Yanga na kuchukua
Kombe, timu yetu ni nzuri na wachezaji wanatulia uwanjani kama
ulivyoona,”alisema.
Stewart aliiwezesha Azam kuwa timu ya
pili nje ya Simba na Yanga kuingia fainali ya Kombe la Kagame, baada ya
Moro United mwaka 2006, ambayo ilifungwa na Polisi Uganda mabao 2-1.
Siku hiyo, rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa hajatimiza mwaka tangu aanze kuishi Ikulu, alikuwepo uwanjani na
aliinuka kushangilia bao la kwanza lililoelekea kubakiza Kombe nyumbani,
ambalo lilifungwa na winga Julius Mrope, hata hivyo Polisi ikifundishwa
na Sam Timbe wakati huo, ilitoka nyuma na kushinda 2-1.

Post a Comment